Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 October 2014
Friday, October 24, 2014

Balaa jingine kwa Balotelli.


Na Oscar Oscar Jr

Kama kwaida Media za nchini Uingereza hazijawahi kushindwa jambo. Kocha wa Cheslea Jose Mourinho na Mshambuliaji wa sasa wa Barcelona, Luis Suarez wamewahi kuwa wahanga wa vyombo hivyo vya habari na kwa sasa, Super Maro Balotelli anakumbana na changamoto hiyo.

Ikiwa na masaa machache tu tangu Balotelli abadilishane jezi na beki wa Real Madrid Pepe, tukio ambao limewakera wapenzi na Uongozi wa Liverpool, jana usiku amekumbwa na mkasa mwingine. Balotelli aliitiwa Polis mahali ambapo alikuwa amepaki gari yake aina ya Ferrari f12.

Ina daiwa kuwa, Balotelli alipaki gari yake na kabla ya kushuka, akatokea mwanamke ambaye baada ya kugundua ni  Balotelli, akaanza kupiga picha gari hiyo kitu kilichomkera mshambuliaji huyo raia wa Italia na kuanza kumrushia dada huyo maneno.

Baadaye mwanadada huyo aliacha kupiga picha na kuamua kupiga picha Polis akidai kuwa, Balotelli amemtishia amani. Polis walikuja eneo la tukio lakini, wahusika wa pande zote mbili bado hawajaliongelea tatizo hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!