Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 November 2014
Saturday, November 08, 2014

Hapa, Mtibwa vs Kagera Sugar kule, Polis Moro vs Prisons


Na Oscar Oscar Jr

LEO katika dimba la Manungu, Turiani kule Morogoro utapigwa mchezo wa ndugu wawili, vinara wa ligi kuu Tanzania bara, Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera. 

Mtibwa ambao hajapoteza mchezo hata mmoja, wanaongoza ligi wakiwa na pointi 14 mpaka sasa huku Kagera wao, wakishika nafasi ya tano baada ya kujikusanyia alama tisa.

Wiki iliyopita Mtibwa walicheza na Simba na kutoka sare ya 1-1 kwenye dimba la Jamhuri Morogoro huku, Kagera Sugar wao walicheza na timu ya Yanga kule Kaitaba na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. 

Mchezo huu utavuta hisia za wapenzi wengi wa soka kutokana na ubora ambao umeonyeshwa na timu ya Mtibwa msimu huu.

Kwa upande mwingine, Polis ya Morogoro leo watakuwa dimbani kuvaana na ndugu zao wa jeshi la Magereza katika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Jamhuri mkoani Morogoro. 

Polis wako nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushinda mchezo moja, sare tatu na tayari wamepoteza mechi mbili.

Tanzania Prisons ambao wametoka kupata sare ugenini dhidi ya Stand United ya mkoani Shinyanga, wanashika nafasi ya 10 baada ya kujikusanyia alama sita. 

Wanahitaji ushindi kwenye mchezo huu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu mzunguko wa kwanza na kuepuka dhahama ya kushuka daraja ambayo walikutana nayo msimu wa uliopita ambapo, walihitaji ushindi kwenye mechi yao ya mwisho ndipo wakasalia kwenye ligi kuu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!