Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 April 2014
Saturday, April 05, 2014

CHELSEA HATIMAYE WARUDI KILELENI



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Chelsea warejea tena kileleni mwa Ligi ya Premia baada ya kujitwalia ushindi rahisi wa 3-0 dhidi ya Stoke City uwanjani Stamford Bridge kwenye mechi ya kuchelewa iliyochezwa Jumamosi.
Mabao ya Mohamed Salah, Frank Lampard na Willian yalitosha kuwawezesha vijana hao wa Jose Mourinho kuwapita Liverpool, ambao watacheza dhidi ya West Ham Jumapili, kwa alama moja.

Ushindi huo pia ulifikisha kikomo mbio za vichapo viwili mfululizo na kudumisha rekodi kali ya Mourinho ambaye hajawahi kushindwa nyumbani kwenye michezo ya Ligi ya Premia.
Ushindi huo pia utawapa motisha vijana hao kabla ya mechi muhimu ya robofainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain, ambapo Chelsea lazima wajikwamue kutoka  kichapo cha 3-1 mechi ya kwanza ndipo wafike nne bora. 

Fowadi wa Uhispania Fernando Torres, ndiye aliyeangaziwa awamu ya kwanza ya mechi baada yake kurejeshwa kwenye timu ya kuanza mechi upande wa Chelsea.
Kichapo cha Jumatano wakiwa Paris kilitokea wakati ambapo Mourinho alikuwa ameanza bila mshambuliaji yeyote anayetambulika na meneja huyo Mreno alilalamika kwamba hana “mastraika halisi”. 

Hakukuwa na shaka kwamba alikuwa akiongea kumhusu Torres, ambaye alipiga kombora la chini ambalo lilitoka nje kwenye goli la Stoke mapema kwenye mechi. Baadaye alinyimwa bao la ufunguzi na kipa Asmir Begovic baada ya mpira wa kifua wa Eric Pieters aliyekuwa akimrudishia kipa kukosa kufikisha mpira huo. 

Lakini mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa £50 milioni ($83m, euro 60m) hakusikika sana tena kwenye kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na wenyeji na kwa mara nyingine alijikuta akizidiwa na wachezaji wenzake waliokuwa na bidii zaidi. 

Salah ndiye aliyefanya kazi zaidi upande wa kulia wa viungo watatu wa kati, ingawa mchango wake wa kwanza ulikuwa kutuma kombora hafifu moja kwa moja hadi mikononi mwa kipa Begovic.
Branislav Ivanovic alituma mpira wa kichwa kutoka kwa kona nje kabla ya Begovic aliyefanyishwa kazi ya punda kutema kombora la kupinduliwa kutoka kwa Willian na jingine la chini kutoka kwa Lampard. 

Torres alihisi alifaa kupewa penalti baada ya kukabiliwa na Geoff Cameron lakini hakupewa. Haukupita muda mwingi hata hivyo kabla ya Salah kujipatia goli lake la kwanza la mchezo na la pili akiwa Chelsea dakika ya 32. 

Nemanja Matic alitoa krosi kutoka kushoto na Mmisri huyo, aliyenunuliwa Januari kutoka Basle, akatoa kombora lililogonga Begovic na kuingia wavuni juu.
Mchezaji huyo wa miaka 21 nusura afunge tena muda mfupi baadaye lakini akapita mpira wakati muhimu, na kuwezesha Begovic kuutwaa. 

Ivanovic alidhani ameongeza la pili kwa mpira mkali wa kichwa baada ya Stoke kupokonywa mpira nusu yao ya uwanja lakini refa akawa macho na akalikataa kwani alikuwa ameotea.
Stoke walikuwa wametishia mara chache upande ule mwingine na walifanya mabadiliko mawili baada ya mapumziko na kuingiza Charlie Adam na Andy Wilkinson. 

Mchango wa kwanza wa Adam ulikuwa kumkanyaga Andre Schurrle, na kumuumiza, lakini refa Lee Probert hakuona hilo.
Schurrle aliondolewa na badala yake akaingizwa Eden Hazard dakika ya 59 na sekunde chache baadaye, Mbelgiji huyo akasaidia kuunda bao la pili. 

Mpira wake wa kurudisha nyuma ulimfungulia mwanya Salah na Mmisri huyo akaangushwa na Wilkinson eneo la hatari.
Begovic alitema penalty ya Lampard lakini kiungo huyo wa kati wa Uingereza akawa wa kwanza kufikia mpira huo na kufungia Chelsea la pili dakika ya 61.

Stoke walijaribu ujanja zaidi kiasi baada ya hapo na wakaanza kupiga kiki za mbali kuelekea kwa goli lililokuwa likilindwa na Petr Cech.
Lakini hakukuwa na matumaini kwa vijana hao wa Mark Hughes baada ya Hazard kwa mara nyingine kumwandalia mpira Willian aliyetoa kombora safi la kujipinda lililombwaga Begovic dakika ya 72 na kukamilisha ufungaji mabao.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!