Uchambuzi: Ndanda vs Mgambo pale Nangwanda Sijaona.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kumtimua kocha wao mkuu Dennies Kitambi, timu ya Ndanda inatarajia kushuka dimbani nyumbani Nangwanda sijaona kucheza dhidi ya Mgambo Shootiong kutoka mkoa wa Tanga.
Hii ni mechi ya pili kwa Ndanda kucheza nyumbani baada ya kuchapwa bao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting wiki iliyopita.
Ndanda walikuwa na mwanzo mzuri sana pale walipoanza ligi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Stand United ugenini Shinyanga lakini vipigo mfululizo vimewaondoa mchezoni vijana hao kutoka Kusini mwa Tanzania.
Nao Mgambo walianza vema kwa ushindi dhidi ya Kagera Sugar wa bao 1-0 lakini baada ya hapo mambo yaligeuka na wiki iliyopita, wametoka kufungwa kwenye Tanga Derby na mahasimu wa Coastal Union.
Msimu uliopita, Mgambo walipata alama sita tu kwenye michezo 13 za mzunguko wa kwanza.
Hayakuwa matokeo mazuri na kocha Bakari Shime atautumia mchezo huu kurejesha ari ya ushindi kwenye kikosi chake.
Pamoja na kupoteza michezo mitatu mfululizo, Ndanda inaonekana kuwa timu yenye safu bora ya ushambuliaji baada ya kufunga mabao saba kwenye michezo minne iliyokwisha cheza.
Kibaya zaidi kinaonekana kwenye safu yao ya ulinzi kwani mpaka sasa, wao ndiyo wamefungwa magoli mengi (tisa) kuliko timu yoyote huku zaidi ya magoli matano, wakifungwa kwa mipira ya set pieces.
Mtokeo ya Ndanda michezo iliyopita.
Standa United 1-4 Ndanda fc
Mtibwa Sugar 3-1 Ndanda fc
Coastal Union 2-1 Ndanda fc
Ndanda fc 1-3 Ruvu Shooting
Matokeo ya michezo ya nyuma ya Mgambo JKT
Mgambo 1-0 Kagera Sugar
Mgambo 0 -1Stand United
Mtibwa 1-0 Mgambo
Coastal 2-0 Mgambo
Ndanda wanatakiwa kuwachukulia Mgambo kwa uzito mkubwa kama timu yenye ubora na uzoefu kuliko wao na hilo linaweza kuwafanya kuwa makini kwa dakika zote za mchezo.
Ndanda wamekuwa hawana uoga kwenye michezo yao kitu kilichopelekea kushindwa kuwazuia wapinzani wao na kukutana na vipigo. Kama watapata ushindi au sare, inaweza kuwa njia ya wao kuanza kujiimarisha upya.
0 comments:
Post a Comment