Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 October 2014
Friday, October 24, 2014

Chicharito harudi tena Old Trafford.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya mechi nne akiwa ndani ya jezi ya "Kifalme' ya Real Madrid, mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez  "Chicharito" amefanikiwa kuwashawishi kocha wa timu hiyo Carlo Anchelotti na Uongozi mzima wa Real Madrid na wanajiandaa kumchukuwa kwa uhamisho wa kudumu mwezi Januari.

Chicharito amefunga magoli matatu sawa na Karimu Benzema ya La Liga na katika mkataba wa uhamisho wa mkopo uliompeleka Real Madrid, gazeti la The daily Express limeeleza kuwa, kuna kipengele kinachoruhusu mchezaji huyo kununuliwa na Real Madrid endapo watamtaka na kuwa tayari kulipa pauni 17 Milion.

Mpaka sasa Christiano Ronaldo anaongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye timu hiyo akiwa ameshafunga magoli 13 na Gareth Bale amefunga manne. 

Chicharito anaonyesha uwezo mkubwa na watoto hao wa kifalme lakini, Real Madrid wanaonekana kusita kulipa kiwango hicho cha pesa ila endapo bei itashuka mpaka pauni 12 Million, kuna uwezekano mkubwa Real Madrid wakamchukuwa kwa uhamisho wa kudumu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!