Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 October 2014
Saturday, October 18, 2014

Uchambuzi: Levante vs Real Madrid leo jioni.




Na Oscar Oscar Jr

 Real Madrid wakiwa wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispani, leo majira ya saa 11:00 jioni watakuwa ugenini kucheza na timu ya Levante kwenye muendelezo wa mechi za La Liga ambazo zinaonekana kurejea baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Tangu Gareth Bale alipojiunga na Real Madrid mwezi Septemba 2013, amekuwa mchezaji aliyepiga pasi nyingi za mwisho kwa Christiano Ronaldo kuliko mchezaji yoyote wa timu hiyo na leo, huenda akaendeleza kazi hiyo kwa Ronaldo amabaye mpaka sasa ndiye anayeongoza kwa ufungaji Hispania akiwa na magoli 13.

Levante ambao wapo kwenye nafasi ya 17 kwenye msimamo wa La Liga, wamefunga magoli manne pekee huku safu ya ulinzi ikiruhusu mabao 15 mpaka sasa. 

Levante wanashika nafasi ya tatu kwenye ligi kuu kwa kuwa na safu mbovu ya ulinzi baada ya kuruhusu magoli 15 nyuma ya Elche waliofungwa mpaka sasa mabao 16 na Deportivo waliokwisha kufungwa magoli 19.

Real Madrid ndiyo timu inayoongoza kwa kuwa na safu bora ya ushambuliaji na mpaka sasa, wamefunga magoli 25 huku mahasimu wao timu ya Barcelona, wakifunga 19 na Valencia 17. 

Carlo Ancelotti ataendelea kumkosa kiungo Semi Khedira na kuna hati hati ya kumkosa pia, beki Sergio Ramos ambaye ameumia mguu na huenda Raphael Varane akachukuwa nafasi yake.

Kikosi cha Levante kinachoweza kuanza leo.
Jesus, Lopez, Rodas, Adoua, Lopez, Morales, Diop, Camarasa, Garcia, Barral, Victor


Kikosi kinachoweza kuanza leo cha Real Madrid
Casillas, Carvejal, Varane, Pepe, Marcelo, Modric, Kroos, Rodriguez, Bale, Hernandez, Ronaldo

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!