Serbia wapewa ushindi na Uefa dhidi ya Albania
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya mchezo kati ya Serbia na Albania kuahirishwa kufuatia vurugu zilizoukumba mchezo huo ambapo chanzo kinatajwa kuwa matatizo ya kisiasa ya nchi hizo, uamuzi umetolewa leo huku Serbia wakipewa ushindi wa magoli 3-0 na chama chama Soka barani Ulaya.
Serbia pia wamenyang'anywa pointi tatu kufuatia wao kuwa chanzo cha vurugu hizo hivyo, hakuna faida yoyote waliyoipata kufuatia ushindi waliopewa. Albania wamenyang'anywa alama kutokana na kugomea mchezo baada ya vurugu kutulia huku waliopewa pia wakinyang'anywa.
Uefa imezipiga nchizo zote mbili faini ya Pauni 78,000 kila nchi kufuatia vurugu hizo huku Serbia wakifungiwa mechi mbili za nyumbani kucheza bila mashabiki.
Nchi hizo zinaonekana kuwa kwenye tofauti za kisiasa tangu miaka mingi na mara ya mwisho kucheza mechi kwa nchi hizo ilikuwa mwaka 1967.
Kwa mujibu wa FA ya Serbia, wao walikuwa tayari kurudia mchezo huo lakini FA ya Albania waligomea taarifa hiyo. Albania ambao walikuwa ugenini, walilalamikia kitendo cha Police na Mashabiki kuwashambulia na kuhatarisha uhai wao.
Mchezo huo wa kufuzu kwa michuano ya kombe la Ulaya, uliahirishwa na mwamuzi kutoka Uingereza Martin Artinkson kwenye dakika ya 41.
0 comments:
Post a Comment