Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 October 2014
Friday, October 24, 2014

Roberto Pires apigwa Uwanjani.


N a Oscar Oscar Jr

Kiungo wa zamani wa timu ya Arsenal, Roberto Pires ameingia kwenye vyombo vya habari baada ya kuenea kwa taarifa za yeye kupigwa wakati wa mapumziko na kocha wa timu pinzani kwenye mchezo wa ligi kuu huko nchini India hapo jana.

Pires ambaye aliichezea arsenal mechi 284 na kufunga magoli 84, amejiunga na klabu ya Goa ya nchini India chini ya kocha raia wa Brazil Zico na jana walikuwa na pambano dhidi ya Atletico de Kolkata ambapo walipoteza mchezo huo kwa kufungwa 2-1.

Katika hali isiyo ya kawaida, Pires amelalamika kupigwa usoni na kusukumwa na kocha Antonio Lopez wakati timu zikiingia kwenye vyumba wakati wa mapumziko. Tayari kocha wa Goa na Uongozi umepeleka malalamiko yao kwenye chama cha soka India ili haki iweze kutendeka.

Indian Super league imezinduliwa msimu huu huku ikishirikisha timu nane na Goa anayochezea Pires, iko kwenye nafasi ya sita baada ya kushuka dimbani mara tatu. 

Beki wa zamani wa Arsenal, Andre Santos ndiye aliyefunga goli la ushindi na kuipatia Atletico de Kolkata pointi tatu muhimu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!