Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 August 2014
Wednesday, August 20, 2014

Pep Gaurdiola sasa kutengua kauli yake



Na Oscar Oscar Jr

Kikosi cha mabingwa wa Bundesliga timu ya Bayern Munich kimeendelea kupata pigo baada kiungo wake wa kutegemewa Bastian Schweinsteiger kuripotiwa kuumia na anadaiwa kukaa nje kwa angalau wiki mbili. 

Bastian Schweinsteiger ni moja kati ya wachezajimuhimu waliosaidia timu ya Ujerumani kuweza kutwaa kombe la dunia na inadaiwa kuwa aliwahishwa kucheza michuano ile kabla ya kupona vizuri.

Si yeye wa pekee kukaa nje kutokana na majeraha Bayern kwani kiungo wa kati mwenzake Javi Martinez atakaa nje kipindi kilichosalia cha mwaka baada ya kuumia kano za goti. 

Difenda Rafinha na kiungo wa kati Thiago Alcantara pia watakaa nje muda mrefu huku Franck Ribery akiwa alikosa kichapo cha fainali Super Cup ya Ujerumani mikononi mwa Borussia Dortmund na ushindi wao wa 4-1 mechi ya raundi ya kwanza Kombe la Ujerumani dhidi ya Preussen Muenster. 

Kocha Pep Guardiola, ambaye mwezi huu alisema hanunui wachezaji wengine, alisema wiki iliyopita kwamba timu hiyo inahitaji mtu wa kujaza nafasi ya Martinez.
Bundesliga inaanza Ijumaa Bayern wakikabiliana na VfL Wolfsburg. 

"Uamuzi wa kama tutanunua au kukosa kununua wachezaji sokoni utategemea mchezaji atakayepatikana na bei yake,” akasema Rummenigge.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!