Na Chikoti Cico
Moja ya mechi ya ligi kuu nchini Uingereza inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka ni kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal mtanange utakaopigwa kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumapili.
Kuelekea mchezo huo kocha wa Liverpool Brendan Rodgers atamkosa mshambuliaji wake Mario Balotelli aliyefungiwa mechi moja na chama cha soka cha Uingereza (FA) pia beki wa timu hiyo Dejan Lovren ana hatihati ya kucheza mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth katikati ya wiki hii.
Liverpool ambao mpaka sasa wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 21 baada ya kufungwa mchezo uliopita dhidi ya United kwa magoli 3-0 wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo kutafuta ushindi kwa nguvu ili kusogea juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.
Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha Liverpool wamekuwa na rekodi mbaya dhidi ya Arsenal kwenye ligi kwani katika michezo 14 iliyopita Liverpool wameshinda michezo miwili tu na kufungwa michezo mitano huku wakitoka sare michezo saba.
Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Jones, Toure, Skrtel, Sakho, Henderson, Gerrard, Lucas, Lallana, Markovic, Coutinho, Sterling.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuelekea mchezo huo atawakosa Laurent Koscieln, Mikel Arteta, Mesut Ozil, David Ospina, Abou Diaby, Jack Wilshere, Aaron Ramsey, Tomas Rosicky na Serge Gnabry ambao ni majeruhi.
Huku pia Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain na Nacho Monreal wakisubiria vipimo vya mwisho kujua kama wako fiti kucheza mchezo huo, wakati huo huo Column Chambers ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu anatarajiwa kurejea uwanjani dhidi ya Liverpool.
Arsenal mpaka sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 26 sawa na Southampton ambao wanashika nafasi ya tano hivyo katika kupigania nafasi ya kurejea “top four” Arsenal wanatarajiwa kupigana kwa nguvu zote ili kuchukua alama zote tatu dhidi ya Liverpool.
Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha mchezaji wa Arsenal Alex Sanchez amehusika katika magoli 11 katika michezo 17 iliyopita ya Arsenal kwenye ligi ya Uingereza ambapo amefunga magoli 11 na kutoa pasi nne za magoli.
Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny, Gibbs, Debuchy, Mertesacker, Monreal, Bellerin, Flamini, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Sanchez, Welbeck,
0 comments:
Post a Comment