Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 October 2014
Thursday, October 30, 2014

Kocha wa Arsenal atangaza mtu wa kuchukua mikoba yake.


Na Oscar Oscar Jr

Katika hali isiyotarajiwa, kuna habari ambazo sio rasmi kuwa kocha wa sasa wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaweza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na tayari mwenyewe ameamua kupendekeza mtu wa kuchukuwa nafasi yake.

Wenger anadaiwa kumpendekeza kocha msaidizi wa klabu ya Real Madrid, Paul Clement. Clement ni kipenzi wa kocha Carlo Ancelotti na amekuwa na tabia ya kuondoka naye kila anapohama klabu moja kwenye nyingine. 

Alikuwa kuwa naye alipokuwa akifundisha timu za  Chelsea, Paris Sait Germany na sasa, yuko naye Real Madrid.

Kama ilivyokuwa kwa kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kupewa nafasi ya kupendekeza mtu wa kuchukuwa nafasi yake pale alipoamua kustaafu, ndiyo inavyosadikiwa kutokea kwa Arsenal. Paul Clement anadaiwa kuwa mzuri sana kwa mbinu ingawa, ukweli ni kwamba hajawahi kupata mafanikio akiwa kama kocha mkuu na hajawahi kuongoza timu kubwa yoyote Duniani.

Taarifa kutoka kwenye magazeti mbalimbali ya Uingereza, yamedai kuwa Arsene Wenger anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu na  Paul Clement ambaye ni Muingereza, anadaiwa kupewa nafasi kubwa ya kuchukuwa mikoba hiyo na mazungumzo yameanza kufanyika. Yanaweza kutokea yale ya David Moyes kwa Manchester United? ni jambo la kusubiri na kuona.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!