Sanchez kurudi na kasi ya ajabu
Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa chile na klabu ya Arsenal Alexis Sanchez anatarajiwa kurudi uwanjani siku ya jumanne pale timu yake itakapokuwa ikimenyana na timu ya Leicester City inayoshika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Sanchez ambaye ameshafunga magoli 18 msimu huu kwenye mashindano yote aliyoichezea timu hiyo alikosekana katika mechi mbili dhidi ya Aston Villa ambapo Arsenal ilishinda magoli 5-0,pia alikosekana katika kichapo cha Arsenal cha magoli 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur jumamosi iliyopita kutokana na kuwa majeruhi.
Akiongea na waandishi wa habari kocha Arsene Wenger alisema kuwa "Sanchez atarudi kwenye timu " aliendelea kusema kuwa" Sanchez ni mfugaji bora wetu na ni mmoja ya mchezaji anayejituma katika timu yetu".
Kuelekea mchezo huo Arsenal itaendelea kumkosa winga wake mahili Alex Oxlade-Chamberlain ambaye ataendelea kuwa nje kwa wiki mbili zaidi ,pia itaendelea kumkosa kiungo wake Jack Wilshere ambaye wiki iliyopita kupigwa picha akiwa katika klabu ya muziki usiku jijini London.
Kwa sas Arsenal inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 42 baada ya kucheza michezo 24,jumanne hii itashuka dimbani kumenyana na Leicester City iliyo nafasi ya mwisho (20) baada ya kukusanya pointi 17 katika michezo 24 iliyocheza mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment