Manchester United wachezea kichapo.
Na Oscar Oscar Jr
Bao la kipindi cha pili lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa Southampton, Dusan Tadic lilitosha kuwapatia Southampton alama tatu muhimu na kurejea kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kuwalaza Manchester United kwa bao 1-0.
Southampton ambao wamejipatia leo ushindi wao wa 12 wa ligi kuu, wanaendelea kuonyesha kuwa wana uwezo wa kumaliza kwenye moja ya nafasi nne za juu.
Nne bora inaonekana kuwa na mvutano mkubwa sana baina ya Sothampton, Arsenal, Liverpool, West Ham United na Tottenham kuwania nafasi ya kuungana na Manchester City na Chelsea ambao bila shaka ndiyo wanaopewa nafasi ya kutwaa ubingwa na hivyo nne bora kwao sio tatizo.
Kipigo hicho cha nne kwa Manchester United msimu huu, kinawaacha kwenye nafasi ya nne wakiwa na alama 37 huku wapinzani wao Arsenal wakipata ushindi kwenye mchezo wa leo wa bao 3-0 dhidi ya Stoke City na kutimiza alama 36 kwenye nafasi tano.
Kwa matokeo hayo sasa Chelsea wanabakia kileleni wakiwa na alama 49 wakifuatiwa na Manchester City wenye alama 47 ambao wanakamata nafasi ya pili baada ya hapo jana kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Everton.
Southampton wanapanda hadi kwenye nafasi ya tatu baada ya kutimiza alama 39 huku Manchester United wakikamilisha nne bora wakiwa na alama 37.
0 comments:
Post a Comment