Rio Ferdinand amesimamishwa kucheza mechi tatu
Na Rossa Kabwine
Beki wa timu ya QPR Rio Ferdinand, amesimamishwa kucheza mechi tatu na kupigwa faini ya pauni 25,000 na chama cha mpira wa miguu cha Uingereza (FA) kwa matamshi yake aliyo andika katika mtandao wa twitter.
Beki huyo wa zamani wa Manchester united, pia amepewa onyo kali kwa tabia yake na ameambiwa kuwa ni lazima akahudhurie katika semina ya mpango wa elimu inayotolewa na chama hicho.
Ina aminika kuwa adhabu hiyo imetokana na maandishi yake ambayo alitumia neno “sket” likiwa na maana ya mshichana au mwanamke mzinzi au mzinifu.
Ferdinand atakosa mechi tatu ambazo ni dhidi ya Chelsea , Manchester city na Newcastle United. Kosa hilo alilifanya Septemba mosi mwaka huu kupitia akaunti yake ya Twitter.
Ferdinand aliandika katika mtanado wa twitter mawazo ambayo yalifikiriwa kuwa yamesababisha adhabu hiyo katika kujibu meseji ambayo ilipendekeza kuwa, timu yake inahitaji beki mwingine wa kati na sio yeye.
Katika kujibu hilo, Rio alijibu “mchukue mama ako ndani, anacheza vizuri sana katika uwanja!#sket(mzinzi)"
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester united, anatumia sana mtandao wa Twitter na tayari ameshatuma tweets zaidi ya 14,000 tangu ajiunge na mtandao huo wa kijamii mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment