Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 August 2014
Thursday, August 07, 2014

Marco Reus bado ni majanga.


 Na Oscar Oscar Jr

Marco Reus ni moja ya vijana wa Ujerumani ambao kwa misimu miwili sasa amekuwa anatajwa kama winga bora kutokana na uwezo wake wa kutengeneza nafasi za mabao na kufunga ambapo msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 16 na kushika nafasi ya tano kwa wafungaji wa ligi ya Bundesliga.

Reus, 25, aliyeumia kwenye goti mkesha wa kuondoka kwa timu ya Ujerumani Juni 7 kuelekea Kombe la Dunia amekuwa nje tangu wakati huo. Bado hakuna matumaini kwa mchezaji huyo baada ya taarifa kutoka wiki hii zikieleza kuwa hatokuwa fiti mwanzoni mwa ligi ya Bundesliga.

Dortmund watafungua kampeni yao ya Bundesliga Agosti 23 dhidi ya Bayer Leverkusen, baada ya kuikabili Bayern Munich katika Super Cup ya Ujerumani Agosti 13 na mechi ya raundi ya kwanza ya kombe Agosti 16 dhidi ya Stuttgarter Kickers inayocheza ligi ya chini. 

Kiungo huyo pia amekuwa akiripotiwa kujiunga na timu mbalimbali barani ulaya na hususani wapinzani wao wakuu wa Bundesliga Bayern Munich. 

Bayern Munich kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na tabia ya kuchukuwa wachezaji wote muhimu wa Borusia Dortmund na kuwasajili. Walimchukuwa Mario Gotze hapo awali na msimu huu tayari wamechukuwa Roberto Lewandowski.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!