Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 August 2014
Thursday, August 07, 2014

Rooney kupewa unahodha pale United?



Na Oscar Oscar Jr

Zali linaonekana kutaka kumuangukia mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney la kuteuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo baada ya meneja mpya Loius Van Gaal kufichua kwamba anapendelea nahodha wa “mtindo wa Kiingereza”. 

Rooney, ambaye ni wa tatu katika orodha ya wafungaji mabao wa klabu hiyo katika historia akiwa na mabao 216, alieleza mapenzi yake ya kutaka kuchukua utepe wa United kwa mpangilio wa kudumu baada ya kuteuliwa kwa Van Gaal. 

Robin van Persie alipigiwa upatu kumrithi nahodha wa awali wa Red Devils Nemanja Vidic, baada ya kuiongoza Uholanzi wakati wa wa kombe la dunia chini ya kocha Loius Van Gaal na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu.

Manchester United inahitaji kufanya mabadiliko makubwa kutokana na kushika nafasi ya saba msimu uliopita baada ya kujikusanyia alama 64. 

Man United walifanikiwa kufunga mabao 64 na kuruhusu wavu wao kutikiswa mara 43 huku Rooney akiibuka mfungaji bora wa klabu hiyo baada ya kufunga mabao 17.

Katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya, Loius Van Gaal kwa nyakati tofauti alionekana kuwatumia Darren Fletcher, Wayne Rooney na Tom Clevery kama manahodha na kufanikiwa kutwaa kombe la bingwa wa kimataifa kwa kushinda mchezo wao wa fainali dhidi ya Liverpool.

Nafasi ya unahodha imebaki wazi kufuatia kwa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Nemenja Vidic kutimkia zake Italia kujiunga na timu ya Inter Millan.

Kumpatia Rooney unahodha linaweza kuwa jambo zuri kutokana na ubora wake kwenye klabu hiyo na kufahamu vema utamaduni wa timu kuliko Roben Van Persie. Rooney ndiye mwenye nafasi kubwa ya kutwaa Unahodha ingawa Loius Van Gaal amekuwa ni kocha asiyetabirika.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!