Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 March 2014
Friday, March 28, 2014

BOSSI WA AC MILLAN AMFAGILIA BALOTELLI.



Kocha wa AC Milan Clarence Seedorf  ameibuka na kusema kuwa,mshambuliaji wake Mario Balotelli bado anaendelea kukuwa kama mchezaji na mwanadamu kufuatia ushindi walioupata siku ya jumatano dhidi ya timu ya Fiorentina kwenye muendelezo wa Seria A.

Baada ya kumpiga bechi mechi iliyopita ambapo Ac Millan walitoka sare na Lazio ya 1-1 ,mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia alikuwa mwiba mchungu sana kwenye mechi yao pale Artemio Franchi huku akipigi mpira wa adhabu kwa ustadi mkubwa na kuiandikia Rosseneri bao na kufanya ubao usomeke 2-0.

Seedorf  alifurahishwa sana na kiwango cha Balotelli, na kudai kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa na mchezo mzuri huku akitekeleza majukumu yake na nidhamu ya hali ya juu kwenye mchezo vitu ambavyo amekuwa akivikosa hapo awali mchezoni.

"Pongeza zimuendee  Balotelli  baada ya mechi yetu na  Fiorentina,amecheza vizuri sana mwanzo mpaka mwisho wa uwanja ndani ya dakika zote 90." Bosi huyo wa Ac Millan aliwaambia wana habari jana ijumaa.


"Nadhani Mario ameonyesha mchezo mzuri kwa pande zote mbili,kama mchezaji na pia kama mwanadamu"

Balotelli ndiye anayeongoza kama mfungaji bora wa timu yake ya  Ac Milan kwenye ligi ya Seria A msimu huu ambapo mpaka sasa ameshafunga magoli 12,lakini kumekuwa na ripoti kuwa klabu inataka kumuuza mshambuliaji huyo kipindi cha majira ya joto kitakapo wadia
.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!