BOSI MTALIANO Carlo Anceloti amesema star wake wa Ureno "anatatizo dogo" na hafikirii kumuweka nje ya uwanja kwenye mechi yake ya La Liga siku ya jumapili na pia,amethibitisha kuwa kipa wake chaguo la kwanza hawezi kumuweka benchi kuelekea mchezo huo.
Bosi huyo wa klabu ya Real Madrid amethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo atakuwa fiti kushiriki mchezo wao na timu ya Rayo Vallecano ambao utachezwa siku ya jumapili ingawa Ronaldo anatatizo kidogo.
Ripoti zimekuwa zikienea kuwa Ronaldo pamoja na kucheza mechi zote za Real Madrid lakini anatatizo kidogo ambalo alilipata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Schalke.
Lakini kocha Anceloti ameendelea kusema kuwa hilo ni tatizo dogo na tatizo litakapo kuwa kubwa ndipo atakapolazimika kumuweka nje star huyo.Kocha huyo mtaliano amesisistiza kuwa,Ronaldo 29 atakuwa mtamboni mwishoni mwa juma hili kama kawaida.
"Christiano amekuwa akifanya mazoezi kama kawaida,sidhani kama tatizo ni kubwa kiasi cha kumuathiri kucheza na kesho atacheza. Ni tatizo dogo sana.aliwaambia wana habari.
Ancelotti ameendelea kusisitiza kuwa,hatomuweka nje kipa Diego Lopez na kumpa nafasi Iker Casillas kutokana na simu anazopigiwa na watu wengi wakilalamikia kiwango kibovu kilichoonyeshwa na golikipa huyo kwenye mchezo wao na Sevilla ambapo Real Madrid walipoteza mechi hiyo.
Anceloti pia amesisitiza kuwa,kiungo Xabi Alonso naye ataendelea kubaki kwenye nafasi yake ingawa hakuwa kwenye kiwango kizuri kwenye mechi mbili zilizopita na kupelekea Real Madrid kuchezea vichapo.
0 comments:
Post a Comment