NIONAVYO MIMI HIZI KAULI ZA WACHEZAJI,ZINA PANDE MBILI.
Na Oscar Oscar Jr.
Mshambuliaji wa Barcelona Alex Sanchez amesema,England haiwezi
kuchukuwa kombe la Dunia 2014 Brazil kwa sababu wachezaji wake ni
laini(soft).
Namwangalia Micar Richards,Namuangali Jack
Wilshere,namuangalia Ashley Cole na upande wa pili namuangalia Wyne
Rooney,nagundua kabisa kwamba,hawa sio "soft" Nampinga Alex Sunchez!
baadae,naangalia madudu
ya Joe Hart,naangalia utu uzima wa Lampard na Gerrard kisha sioni
mbadala wa hao watu.Nikifika kwenye hii point,nakubaliana na Sanchez!
Steven Gerrard kasema,Luis Suarez ni mshambuliaji hatari zaidi kuliko
Torres ukichezanae.Anadhani ubora wa Torres yule wa liverpool huwezi
linganisha na Suarez.
Nikimkumbuka El-nino yule mwekundu namna alivyokuwa analijua goli,nampinga Gerrard.
Baadae nakumbuka kwamba,Torres alicheza zama za Alonso Original na
Gerrard Original na kwa sasa,Suarez anacheza kwa Gerrad fake na
Henderson Fake.Nikifikia hii point,nakubaliana na Gerrard.
I'm sorry!
15 November 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment