NIONAVYO MIMI MTOTO WA TABORA:
FACEBOOK NA TWITTER ZINAWEZA KUONGEZA UTAMU WA SOKA.
Na Oscar Oscar Jr
Klabu za VPL ambazo zinatumia mitandao ya kijamii kama Facebook na
Twitter wanakosa ubunifu,ndiyo maana hawana followers wengi online
wakati huku mtaani kwenye "Hard copy" wana maelfu ya Fans!!
Unajui kwa nini? Shabiki haoni taarifa mpya na zakuvutia thats why haoni
sababu ya ku-like au ku-follow account hizo.hivi leo ukisikia kwamba
Haruna Moshi na Jerry Santo watakuwa wanajibu maswali ya mashabiki wao
kuanzia saa 2-4 usiku kwenye Twitter account ya Coastal union,utalala?
Utaacha ku-like page yao?
Mashabiki wanahamu ya kuwajua
wachezaji wao kiundani,wanatamani kujua maisha binafsi ya wachezaji n.k
Hivi leo Yanga wakimuweka Manji "live" kwenye Facebook account ya Yanga
na kujibu hoja za mashabiki kwa masaa mawili tu,unadhani kunamtu
atalala? Unadhani kuna mtu ataacha ku-like ukurasa wao?
Tuwekeni LIVE na wachezaji wetu,tujue mengi kupitia majibu yao.Kazi yenu
kubwa kwenye account hizo ni kutuwekea kikosi kitakachoanza na vipicha
uchwara!! Hivi Simba mnashindwa nini angalau kumleta Abel Dhaira LIVE
tuzungumze naye??
Waleteni wachezaji karibu na mashabiki ili kupunguza hata uongo ambao tunauona kwenye baadhi ya Media.
I'm sorry!
15 November 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment