NIONAVYO MIMI KUFUATIWA KUFUNGIWA KWA BAADHI YA VIWANJA NCHINI.
Na Oscar Oscar Jr.
Huwa inatokea mzozo sana kwa sisi tunaokaa nyumba za kupanga,unataka
kupakiwa rangi chumba chako,mwenye nyumba hana time! Unataka kufungiwa
feni,mwenye nyumba hana time! Mwisho unaamua ama ubaki hivyo hivyo au
ukatafute nyumba nyingine ukapange!!
Kamati ya Bodi ya Ligi imevifungia baadhi ya viwanja kutokana na kutokuwa na ubora lakini
viwanja hivi ni mali ya Chama Tawala na chama tawala hakina mpango wa
kuviboresha,na timu zinazokodi viwanja hivi,hazina mpango wa kujenga vya
kwao.Hapa patamu sana!!
Simba na Yanga wanaweza wakawa
wanacheka tu kwa sababu jambo hili haliwaathiri,ila tukibadili mawazo
tunaweza tukagomea uwanja wa Taifa nao upumzishwe ili sisi wa mikoani na
nyie wa kiriakoo,wote tukawapigie magoti Azam pale Chamazi!!
Hivi nani anatakiwa kuviboresha ni TFF,Chama Tawala au timu zinazolipia kodi kila wanapovitumia??
Natamani kusikia mwenyekiti wa hicho chama akisema kuwa hawatoviboresha
kwa sababu chama kinataka kuanzisha mradi wa kuku,hivyo basi wapenda
mpira wajenge vya kwao!!
I'm sorry!
15 November 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment