Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2013
Friday, November 15, 2013

JAMAL MALINZI AANGALIE MBELE NA NYUMA PALE TFF!

NIONAVYO MIMI KWENYE ARI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA.

Jamal Malinzi kwa sasa muache atimue watu ambao sio maswaiba wake,baadae ataanza kutimua watu ambao ni maswaiba wake na mwisho,atatimuliwa yeye mwenyewe na watanzania!!

Unajua kwa nini? Soka letu halina tofauti na wanafunzi wa darasa la saba ambao walifaulu mtihani kwenda kidato cha kwanza kumbe hawajui kusoma na kuandika.Unadhani wanaweza kufika chuo kikuu?

Tanzania bado tuna amini kila mtu ni kocha wa mpira,kila mtu ni refa,kila mtu ni kamisaa na mpira anaweza kucheza mtu yoyote.Hapa ndipo tunatakiwa kuanza kupabadilisha.

Unakumbuka baada ya JK kitimua safu ya mzee Beny? Beny alijiweka pembeni.Ninachokiona hapa ni Mzee Tenga na yeye atajiweka kando.Bado tunahitaji msaada wa Tenga kwenye soka letu.

Watanzania watakapo taka kwenda AFCON 2015 Morocco,hapo ndipo patakapo chimbika Mr President!

I'm sorry!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!