Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans
leo imetuma salaam kwa timu ya Azam ambayo watakutana siku ya jumamosi
katika mchezo wa Ngao ya Hisani baada ya kuichapa Sports Club Villa ya
Uganda mabao 4-1.
Ikiwa na wachezaji wake wapya Yanga iliingia uwanjani kwa lengo la
kuhakikisha inaendeleza wimbi lake la ushindi, ikizingatia ndio timu
yenye kikosi bora kabisa kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati.
Mshambuliaji aliyerejea Yanga akitokea klabu ya Azam FC,
msimu uliopita akichezea Simba SC Mrisho Ngassa aliipatia timu yake bao
la kwanza dakika ya saba ya mchezo kwa shuti kali la kimo cha mbuzi
lililomshinda mlinda mlango wa SC Villa Elugant Martin akiduwaa asijue
la kufanya.
Dakika ya 18 ya mchezo mshambuliaji Ndaula Moses
aliipatia SC Villa bao la kusawazisha kwa kichwa kufuatia krosi
iliyopigwa na Ronald Muganga kumkuta mfungaji na kuukwamisha mpira
wavuni huku walinzi wa Yanga wakitegeana na kumtazama mfungaji.
Nahodha
wa timu ya Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' aliipatia timu yake bao la
pili kwa mkwaju mkali kufuatia mpira wa adhabu aliosogezewa na Haruna
Niyonzima kumshinda mlinda mlango wa SC Villa akiwa amesimama na mpira
kujaa wavuni na kuhesabu bao la pili kwa watoto wa Jangwani.
Dakika
tatu baaadaye dakika ya 30, mshambuliaji Didier Kavumbagu aliipatia
Young Africans bao tatu akimalizia mpira uliopigwa na Jerson Tegete
kugonga mwamba wa juu na kumkuta Kavumbagu aliyeukwamisha wavuni mpira
huo.
Mpaka timu zinakwenda mapumziko, Young Africans 3- 1 SC Villa.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na katika dakika ya 62 ya mchezo kiungo
Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao nne kwa ustadi wa hali ya
juu akiitumia vizuri pasi aliyopewa na mshambuliaji Huseein Javu na
kuufanya ubao wa matanagazo usomeke 4-1.
Yanga ilifanya mabadiliko
amabapo waliingia Rajab Zahir, Hussein Javu, Bakari Masoud, Said
Bahanuzi na Oscar Joshua kuchukua nafasi za Kelvin Yondani, David
Luhende, Athuman Idd 'Chuji', Jerson Tegete na Haruna Niyonzima.
Hussein
Javu nusura aiipatie Young Africans bao la dakika ya 72 ya mchezo baada
ya mpira alioupiga kugonga mwamba wa juu kabla ya kuokolewa na walinzi
wa SC Villa ya Uganda.
SC Villa
ilijaribu kusaka mabao lakinu umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa
kikwazo kwao muda wote wa mchezo huku golikipa Ally Mustapha 'Barthez'
akikoa mabao mawili ya wazi kutoka kwa mshabuliaji Ronald Muganga.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 4 - 1 SC Villa.
Mara
baada ya mchezo wa leo kikosi cha Young Africans kitaendelea na mazoezi
kesho asubuhi katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola kujiaanda na
mchezo wake wa Ngao ya Hisani dhidi ya wana lambalamba timu ya Azam FC
mchezo utakaochezwa tarehe 17.08.2013 katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam
Young Africans: 1.Ally Mustapha
'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende/Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub
'Cannavaro' 5.Kelvin Yondani/Rajab Zahir, 6.Athuman Idd 'Chuji/Bakari
Masoud, 7.Mrisho Ngassa, 8.Salum Telela, 9.Jerson Tegete/Hussein Javu,
10.Didier kavumbagu, 11.Haruna Niyonzima/Said Bahanuzi
0 comments:
Post a Comment