Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji ameitisha mkutano wa dharura wa wanachama tarehe
18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA
saa 3.30 asubuhi kujadili sakata linaloendelea kuhusu michezo ya Ligi
Kuu kurushwa katika kituo cha Azam TV.
Yanga ilitoa msimamo wake wa
kupinga michezo inayoihusu kurushwa na kituo hicho huku TFF ikisisitiza
maamuzi yaliyofikiwa na kamati ya ligi na wawakilishi wa klabu nyingine
wakiiponda Yanga.
Sehemu ya barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari
inasema "Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu
kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa
mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala
hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa
maslahi ya Klabu yetu".
0 comments:
Post a Comment