Searching...
Image and video hosting by TinyPic
11 July 2013
Thursday, July 11, 2013

PIGO MAN UNITED WAKIPATA MAPOKEZI MAZURI THAILAND, THIAGO ALCANTARA AAMUA KUMFUATA GUARDIOLA BAYERN MUNICH


KIKOSI cha Manchester United kimetua Bangkok na kupata mapokezi mazuri leo asubuhi, lakini wakiwa na msongo wa mawazo kutokana na habari kuhusu Thiago Alcantara.
Ilifikiriwa kwamba kiungo huyo wa Barcelona amechagua kujiunga na United baada ya kuamua kutafuta timu itakayomuwezesha kujenga nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha Hispania kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani kwa kuondoka Nou Camp.
Pamoja na hayo, sasa inaripotiwa nchini Hispania kwamba Thiago ameona bora kwenda kuungana na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola huko Bayern Munich.
Arrival: Manchester United landed in Bangkok as they prepare to get their pre-season underway
Wanawasili: Manchester United wamewasili Bangkok kujiandaa kwa msimu mpya
Rio Ferdinand
Wayne Rooney
Sare sare: Rio Ferdinand (kushoto) na Rooney kulia
Arrival: Manchester United landed in Bangkok as they prepare to get their pre-season underway

RATIBA YA ZIARA YA KUJIANDAA NA MSIMU

Julai 13 na Singha All Star XI (Uwanja wa Rajamangala, Bangkok - Kombe la miaka 80 ya Singha) saa 8mchana
Julai 20 na A-League All Stars (Uwanja wa ANZ, Sydney) sa 4.30asubuhi
Julai 23 na Yokohama F-Marinos (Uwanja wa Nissan, Yokohama) saa 5.20asubuhi
Julai 26 na Cerezo Osaka (Uwanja wa Osaka Nagai, Osaka) saa 5asubuhi
Julai 29 na Kitchee (Uwanja wa Hong Kong, Hong Kong) saa 7mchana
Ikithibitika, habari hizo zitakuwa pigo kwa kocha David Moyes, ambaye alitumai kumtumia Thiago kuimarisha safu yake ya kiungo, kufuatia kustaafu kwa Paul Scholes na huku Darren Fletcher na Anderson wakiwa hawako sawa.
Mabingwa hao wa England, Manchester United watacheza mechi tano za kirafiki katika ziara yao hii ya Mashariki ya Mbali na Australia, wakianza na Singha All Stars Jumamosi kujiandaa na msimu mpya, wakiwa chini ya kocha mpya, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
Flashpoint: The United squad was bombarded with cameras as they land in Bangkok
kamera kamera: Kikosi cha United kilipokewa na kamera kilipotua Bangkok
Girls just wanna have fun: Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
Vimwana sasa: Mashabiki wa Manchester United wakiwakaribisha wachezaji wao walipotua Thailand
Manchester United fans welcome the players as they land in Thailand
New beginnings: David Moyes will get his first look at his new charges after taking over at United
New beginnings: David Moyes will get his first look at his new charges after taking over at United
Mwanzo mpya: David Moyes ataanza kazi rasmi baada ya kuchukua mikoba ya ukocha United
Tribute: Moyes pays respect to the monarch at Siriraj Hospital in Bangkok ahead of United's tour
Moyes akiwa katika hospitali Siriraj mjini Bangkok 
Respect: Moyes and Ryan Giggs stand next to the image of Thai King Bhumibol Adulyadej and Queen Sirikit
Heshima: Moyes na Ryan Giggs wakiwa wamesimama pembeni ya picha za Mfalme wa Thai, Bhumibol Adulyadej na Malkia Sirikit

Baada ya kuondoka Uwanja wa Ndege, Moyes na wachezaji wake walikwenda kutoa heshima zao katika hospitali ya Siriraj mjini Bangkok. Kocha alisimama na Ryan Giggs pembeni ya picha za Mfalme wa Thai, Bhumibol Adulyadej na Malkia Sirikit.
Kwanza Moyes akiwa na Ryan Giggs ambaye sasa ni kocha mchezaji, walisaini kitabu cha salamu nzuri kwa Mfalme wa Thai, ambaye anapendwa sana nchini humo.
Pia wachezaji wa United waliruhusiwa kupumzika kwa muda baada ya saa 12 za kuwa angani kwenye ndege, na baadaye watafanya mazoezi katika Uwanja ambao milango yote itafungwa.
Kutokana na Robin van Persie kukosa mechi hii katika ziara hii, ambayo itaendelea Australia Jumapili kabla ya kutua Yokohama, Osaka na kumalizia Hong Kong Julai 29, Wayne Rooney ataanza kama mshambuliaji wa kati.
Welcome: The United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Karibu: Kikosi cha United kimepokewa vizuri Bangkok
Welcome: The Manchester United squad are greeted by passionate fans in Bangkok
Karibuni: Manchester United walivyopokewa Bangkok
Smile for the camera: Rio Ferdinand ensures he'll have plenty of memories from the trip to Thailand
Tabasamu la kamera: Rio Ferdinand akipiga picha za video Thailand
Wilfried Zaha
Manchester United football player Ryan Giggs
Wakongwe: Ferdinand (kushoto) na Ryan Giggs kulia
Thiago Alcantara
Pep Guardiola
Pigo: Thiago Alcantara (kushoto) inadaiwa ameamua kwenda kuungana na kocha wake wa zamani, Guardiola (right) huko Bayern Munich

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!