KALI YA LEO: MTANDAO WA KUUZA BIDHAA ZA CHELSEA WATANGAZA KIMAKOSA BIDHAA ZA ARSENAL NDANI YA MTANDAO WAO
Kulikuwa na sura zisizo na furaha leo pale Stamford Bridge asubuhi ya leo baada ya mtandao rasmi wa mauzo ya bidhaa za Chelsea huko USA kuweka tangazo la bidhaa za Arsenal kwenye mtandao huo.
Mtandao huo ambao ni kama duka la online upo maalum kwa ajili ya mashabiki wa kimarekani wa Chelsea - leo mapema asubuhi uliweka tangazo la kuuza nguo za watoto zenye nembo kubwa ya Arsenal kwa bei ya $16.99, huku kukiwa na maelezo yafuatayo:
'The have won 13 First Division and Premier League titles and 10 FA Cups. They are your Gunners. Show your support in this cool, unique tee. 100% cotton tee with a tagless design for added comfort.'
Lakini baada ya muda kidogo tangazo hilo lilitolewa na inaaminika lilikuwa ni kosa la kampuni ya Sports Endevours, ambayo ndio inaendesha maduka ya online ya vilabu vya Arsenal na Chelsea huko USA, ingawa pia kumekuwepo na taarifa kwamba kulikuwepo na mchezo wa 'hacking' uliofanywa na wahuni wa internet. Lakini unaweza kuliona tangazo kama hilo kwenye mtandao huu Arsenal USA store.
0 comments:
Post a Comment