Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 May 2013
Thursday, May 30, 2013

TFF NA WACHEZAJI WA KIGENI


Wachezaji wageni Ligi Kuu kubanwa

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litakutana na klabu za Ligi Kuu kuzikumbusha azimio la mwaka jana la mjini Bagamoyo kuhusu wachezaji wa kigeni.

Azimio hilo lilipitisha sheria inayokataza klabu za Ligi Kuu kusajili zaidi ya wachezaji watatu kutoka nje ya nchi.

Pamoja na sababu mbalimbali za kupitisha azimio hilo, dhamira kuu ilikuwa kuwapa fursa wachezaji wa ndani kuonyesha vipaji vyao kwenye michuano ya ligi.

Kwa sasa, klabu zinaruhusiwa kusajili siyo zaidi ya wachezaji watano kufikia msimu uliomalizika, lakini kama azimio hilo litaungwa mkono na klabu, basi msimu wa 2013/14 utashuhudia wachezaji wachache wa kigeni.

Klabu za Simba, Yanga na Azam ndizo zinaoongoza kusajili wachezaji wa kigeni kulinganisha na timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo.

Mtendaji Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alikaririwa na mtandao wa soka nchini Uganda, akisema mchakato huo unaendelea kufanyiwa kazi na watakutana na viongozi wa klabu kujadili.

“Ni sheria mpya ya Azimio la Bagamoyo. Ni vyema sheria zilizowekwa na sisi wenyewe zikaheshimika. Tutakutana na klabu kujadili azimio hili,” alisema Osiah.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!