Luke Shaw ampa shavu De Gea
Na Oscar Oscar Jr
Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw, ameibuka na kudai kuwa, uwezo ulionyesha jana kipa wa timu yake David De Gea ni kiwango cha Dunia. Mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford ilimalalizika kwa sare ya 1-1 huku Thibout Courtois wa Chelsea akitangazwa nyota wa mchezo huo.
Courtois alikuwa jushaa pale alipofanikiwa kuokoa michomo kidhaa iliyopigwa na mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie.
Akizungumzia uwezo wa Courtois, Shaw anasema, ni kipa ambaye alionyesha uwezo mkubwa sana tangu akiwa na klabu ya Atletico ambapo msimu uliopita walitwaa ubingwa wa La Liga na kutinga fainali ya Uefa na kupoteza mbele ya Real Madrid.
Kipa wa Manchester United alifanya kazi nzuri sana hasa pale alipookoa mkwaju wa mbali kutoka kwa mshambuliaji Didier Drogba na Eden Hazard ambaye alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwapa Chelsea bao la kuogoza baada ya kuwatoka mabeki wa United na De Gea, akaokoa dhahama hiyo.
Pamoja na makipa hao kufanya vizuri kwa nyakati tofauti, Luke Shaw ana amini baada ya muda fulani, David De Gea atakuja kufanya mambo makubwa sana.
0 comments:
Post a Comment