Umiseta kwa sasa imerudi nchini kwa kasi sana .ila imerudi muda ambapo nchi ipo kwenye urasimu mkubwa katika soka.kwanza fitina baina ya vilabu ni kubwa,pili majungu mengi na tatu majukumu kupangwa/kupangiwa na wakubwa .
Hapa ndipo umiseta inajikuta katika balaa uchaguzi wa wachezaji kupitia walimu umekuwa wa kirasimu sana.watoto wenye vipaji waliachwa sana.na kuchukua wasiojua.
Pia baada ya umiseta wachezaji husika huachwa bila kufuatiliwa na kuendelezwa na huchukuliwa watoto ambao si wanafunzi na wa umri mkubwa ndo hushiriki wakati si walengwa kwenye kuunda timu ya mkoa.ni vigumu kuwapata kina zinedine zidane wa kitanzania kwa hali hii.
matumizI mabaya ya fedha za umiseta kwa waliopewa dhamana ya kuzitumia.hawazitumii kwa malengo husika.binafsi kungekuwa na chombo cha kuendesha umiseta kama copa coca cola nadhani ingekuwa poa sana.
0 comments:
Post a Comment