Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 May 2013
Tuesday, May 28, 2013

MPIRA NI MALI,HAIHITAJI MAANDAMANO KAMA YA GESI MTWARA.


Hivi karibuni taarifa zimetoka kwamba Radamel Falcao anakwenda Monaco FC timu ambayo imepanda daraja na kushiriki ligi kuu nchini ufaransa msimu ujao.Hapa ndipo utakapojua kwamba mpira ni biashara na mashabiki ndo wateja.

Mbeya city imepanda daraja na itacheza vodacom premier league msimu ujao.hivi kama wangetoa pesa na kumnunua mtu kama Haruna Niyonzima wangetengeneza pesa kiasi gani? Wangeongeza mashabiki kiasi gani uwanjani?

Watu wanajaa sana uwanjani mechi za simba na Yanga moja ya sababu ni,ndiko waliko wachezaji wakubwa ila kama watapatikana hata pale Tabora kwa Rhino Rangers iliyopanda daraja,uwanja wa Ali Hassan Mwinyi utafurika tu.

Ashanti united nayo imetinga VPL msimu ujao kama wanapata watu wawili kama Shomari kapombe na Mwinyikazi moto,wanaweza kuandaa bidhaa za hao watu kuanzia ya shilingi mia tano hadi elfu ishirini.Unadhani hadi mwisho wa msimu watakusanya shilingi ngapi?

Mashabiki wanapesa kuliko mtu yoyote,Toto Africa Imeshuka daraja lakini kama wanamnunua mtu kama Kelvin Yondani na Juma Kasseja lazima wavune pesa tu kama wanajua kuwatumia kibiashara.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!