Kapteni wa Manchester City, Vincent Kompany, amedumisha matarajio ya
uwezo wa timu hiyo kushinda ligi ya Premier ya Uingereza baada ya kikosi
chake kuwaadhibu majirani zao Manchester United 3-0 Jumanne.
Ushindi huo uliwainua kufunga mwanya kati yao na Chelsea
wanaoshikilia nafasi ya kwanza hadi alama tatu na mechi mbili za huku wakiwa na mechi 2 mkononi.
Kompany alisisitiza bado ni mapema kuwavisha taji hilo huku mechi
kadhaa zikisalia ikiwemo safari yao ya Jumamosi kumenyana na Arsenal katika dimba la Emirates.
“Hii ilikuwa hatua moja tu na timu zingine zina ubora bado na hadi
wakati ule tutazoa alama zote, sitakubali kuona kuwa ndo tumefika,” mlinzi huyo
wa Ubelgiji alinena.
0 comments:
Post a Comment