Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 January 2015
Wednesday, January 21, 2015

Masau Bwire afunguka sakata la Amisi Tambwe kukabwa.


Na Masau Bwire


Mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya Yanga na Ruvu shooting, madai ya Yanga kwamba walifanyiwa fujo na Ruvu shooting je, yanalenga nini?

Yanga ilicheza faulo 16, Ruvu shooting 11. Nani anastahili kulalamikiwa kwa mchezo mbaya? Wamekomalia Tambwe kanigwa, katukanwa, kachezewa rafu, wanaliona hilo tu, waliyofanya wao hawayaoni!

Tambwe kamkanyaga makusudi George Osei mpaka kaenda chini, kampiga ngumi kipa wetu, Yondani kamkanyaga makusudi Abdulhaman Musa tena ndani ya 18, ilikuwa penalti ya wazi lkn ikafunikwa, Msuva kamkanyaga makusudi Hamis eneo la hatari huyo nayo ikafichwa!

Makosa yanaonekana ya Ruvu shooting ya Yanga hayaonekani japo ndio waliocheza rafu zaidi ya Ruvu shooting au ndo ile ya Kanya bata, kuku kajisaidia?

Hata ktk kadi za njano, Yanga wamepewa wachezaji watatu, Kelvin Yondani, Hamis Tambwe na Simon Msuva. Ruvu shooting wamepewa mbili, Salvatory Mtebe na kipa Abdallah Shabani kwa kuchelewesha mpira. Hapa nani kacheza rafu zaidi ya mwenzake?

Kilichopo hapa, nadhani Yanga wanajaribu kuwaadaa washabiki wake kwa mwenendo wa timu kutofanya vizuri ili kukwepa lawama na kujaribu kutafuta visingizio kwa mambo ambayo hayapo!

Mnakumbuka mwanzoni Yanga walidai Ruvu shooting walikuwa wakijiangusha na kupoteza muda hali iliyowafanya wakose ushindi ktk mchezo huo.

Walipoona hoja hiyo haina mashiko, wakatunga hii waliyonayo kwa sasa wakidai eti Ruvu shooting walitumia mbinu za boko haram na Al shabab, kuwafanya wakose ushindi!

Hivi, mtu anayejiangusha ana jeuri kweli ya kumkaba mtu na kutumia mbinu za hayo makundi ya kivita wanayoifananisha na Ruvu shooting?

Sijui wewe una maoni gani ktk tukio hili?
Naomba kama upo uwezekano, uchukuliwe mkanda wa video uonyeshwe hadharani watu wapate ukweli wa haya yanayozungumzwa.

Picha za mnato, ni sawa lkn uhalisia wa tukio ni mkanda wa video. Azam tv, clouds tv, tuwekeeni mambo haya hadharani! Masau ambaye ni msemaji wa Ruvu Shooting ameandika makala hiyo ya ufafanuzi na kuituma kwenye moja ya makundi ya michezo kupitia Whatsaap.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!