Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 December 2014
Monday, December 08, 2014

Manchester United yaichapa Southampton,yatua nafasi ya tatu.



Na Florence George


Hali imemeendelea kuwa mbaya kwa klabu ya Southampton pindi inapocheza dhidi ya timu kubwa katika ligi kuu nchini Uingereza msimu huu mara baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 toka kwa Manchester United mchezo uliochezwa siku ya jumatatu usiku katika uwanja wa St Mary's.

Ulikuwa mchezo wa kwanza kuwakutanisha makocha Waholanzi ambao wapo katika bifu kubwa ,Louis Van Gaal wa Manchester United na Ronald Koeman wa Southampton ambayo wameshawahi kufanya kazi pamoja katika timu ya Ajax ya nchini Uholanzi mwaka 2004.

Katika mchezo huo kocha Van Gaal aliendelea kutumia mfumo wake wa kuchezesha mabeki watatu huku akijaza viungo sehemu ya katikati ya uwanja ambayo kijana Paddy McNair alianza sambamba na Marcos Rojo pamoja na Chris Smalling ambaye aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na John Evans aliyerejea toka majeruhi.

Mshmbuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ndie alikuwa shujaa wa United baada ya kufunga magoli yote mawili, huku goli kipa wa kimataifa wa Hispania David Degea akiendelea kudhihirisha ubora wake baada ya kuokoa michomo mbalimbali ikiwamo ya Graziano Pelle pamoja na Nathaniel Clyne.

United ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 12 mara baada ya beki Jose Fonte kupiga pasi mbovu iliyonaswa na Van Persie kisha kufunga goli hilo,baada ya mashambulizi ya kupokezana mshambuliaji wa Southampton Graziano Pelle alifanikiwa kuisawazishia timu yake katika dakika ya 31,hivyo timu kwenye mapumziko zikiwa zimefungana 1-1.

kipindi cha pili kilianza kwa kasi na ilikuwa United iliyofanikiwa kupata goli ya pili dakika ya 71 mfungaji akiwa Van Persie tena akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Wayne Rooney,hivyo hadi mwisho wa mchezo matokeo kubaki hivyo hiyo huku United ikiondoka na pointi zote tatu.

Ulikuwa ushindi wa tano mfululizo kwa United huku Southampton ikipoteza mchezo wake wa tatu mfululizo baada ya awali kufungwa na Manchester City na Arsenal.

Kwa matokeo hayo,sasa Manchester United imepanda hadi nafasi ya tatu la ligi hiyo kwa kufikisha pointi 28 katika michezo 15, pointi tano yuma ya mahasimu wao Manchester City yenye pointi 33 katika michezo 15 iliyocheza huku ikizidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo timu ya chelsea yenye pointi 36 katika michezo 15 iliyocheza mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!