Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 December 2014
Monday, December 08, 2014

Je, Danny Mrwanda alihitajika Yanga Sc?




Na Samwuel Samuel 
0652-404525

Wakati matajiri wa darajani nchini England wanamleta Samuel Eto'o katika ligi ya Barclay's wapo waliobeza , wapo waliokaa kimya wakisubiri matokeo ya uwanjani ndo waongee na wapo walioamini Etoo angeisaidia Chelsea katika miaka 30 aliyokuwa nayo wakati ule. 
  
 Mcameroon yule alifanya yake na kuondoka zake. Mourinho hakuchoka akamleta Drogba ambaye naye anathibitisha ubora wake katika miaka 31. Mchezaji yoyote yule ambaye anacheza katika kipaji halisi na kuzingatia miiko ya soka hudumu kwenye mchezo huo kwa muda mrefu

Tanzania yetu tumezoea kuona wachezaji wanaitwa mafaza au maveterani wa soka katika miaka 25, 26 na 27 tu wakati kwa wenzetu ndo mchezaji anakuwa katika kilele cha mafanikio yake. Tafuta umri wa Cristiano Ronaldo,Lionel Messi, Iniesta, Kaka n.k utaelewa hilo. Wachezaji wetu hawajui thamani ya kulinda vipaji vyao, wanalewa sifa mapema na kupotea . 

Tegete ana miaka 26 tu lakini sidhani kama ana jipya sasa zaidi ya kubebwa na historia. Wengine ni mfumo mbaya wa vilabu vyetu unawamaliza kisoka. Usajili usio na malengo na siasa chafu katika soka. Singano anaanza taratibu kuondoka kwenye ramani ya soka wakati bado kijana mdogo na mwenye kipaji hasa. 

Yupo wapi Amir Maftaa? Kiggy Makasi? Mtazame Abuu Mtiro, huyu beki alikuwepo 2001 wakati Yanga ikifungwa 4-1 kombe la tusker na Simba lakini amejitunza kwenye game leo hii anaitwa kuchezea timu ya taifa akitokea Kagera Sugar

Hiyo inaonesha thamani ya kujitunza na kuzingatia miiko ya soka. Madaraka Selemani " mzee wa kiminyio" alitundika daruga akiwa na miaka 40 kama sijakosea. Inasadikika ndiye fowadi aliyedumu kwa muda mrefu kwenye soka nchini Tanzania.

Hivyo basi msishangazwe na usajili wa Danny Mrwanda akiwa na miaka 31 tu. Tafuteni historia ya mchezaji huyo toka akiwa AFC ya Arusha, Simba SC na baadae kule Vietnam alipocheza soka la kulipwa. Kote huko amecheza kwa mafanikio na hakuna kocha aliyebeza uwezo wake.

 Msimu huu akiwa na timu ya Polisi Moro  isiyo na viungo mahiri wa kutengeneza pasi nzuri kama walivyo viungo Simba SC, Azam FC na Yanga lakini Mrwanda ametikisa nyavu mara nne na goli moja akiipangua ngome imara ya Simba SC. 

Wahenga wanasema thamani ya mvinyo huongezeka kadri unavyozidi kukaa. Danny mwenye kasi, nguvu na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira nadhani kwa mara nyingine anakutana na timu yenye viungo bora kabisa nchini kutaradadi kipaji chake. 

Mtazame Niyonzima, Msuva, Ngasa, Twite, Seme, Emerson, Dilunga na Nizar Khalfan achilia mbali Hamisi Thabiti, Telela na Said Juma. Wote hao ni wazuri kumtengenezea pasi nzuri kucheka na nyavu. Kikubwa ni mfumo wa Maximo tu umtengenezee mazingira mazuri mkongwe huyo kucheka na nyavu. 


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!