Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 November 2014
Sunday, November 23, 2014

Uchambuzi: Crystal Palace vs Liverpool



Na Chikoti Cico

Katika mwendelezo wa ligi kuu nchini Uingereza leo hii timu ya Crystal Palace itaikaribisha Liverpool kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Selhurst Park.


Mchezo kama huu kwenye msimu uliopita uliowanyima Liverpool ubingwa baada ya kutoka sare ya magoli 3-3 huku Palace wakirudisha mgaoli yote matatu ndani ya dakika tatu za mwisho wa mchezo.

Crystal Palace ambao wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na alama tisa wanatarajia kuingia kwenye mchezo huo kutafuta ushindi kwa nguvu zote ili kujiondoa kwenye mlolongo wa kushuka daraja hasa baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabovu.

Akiwa ameshinda michezo miwili tu na kutoka sare michezo mitatu huku akifungwa michezo sita kati ya michezo 11 kocha wa Crsytal Palace Steve Warnock ana kibarua kigumu katika kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa tatu muhimu ugenini.

Wakati huo huo kocha huyo atamkosa James McArthur aliyeko majeruhi ila kurejea kwa nahodha Mile Jedinak aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu kutaiongezea nguvu safu ya kiungo ya Palace kwenye mchezo huo.

Kikosi cha kocha Warnock kinaweza kuwa hivi: Speroni; Mariappa, Delaney, Dann, Ward; Puncheon, Ledley, Jedinak, Bolasie; Chamakh, Campbell.

Kwa upande Liverpool maarufu kama majogoo wa jiji hali sio nzuri kwenye safu yao ya ushambuliaji baada ya Daniel Sturridge kuumia tena huku Mario Balotelli nae akiwa na hati hati ya kucheza mchezo huo baada ya kuumia kwenye michezo ya kimataifa akiichezea Italia hivyo Rick Lambert anabaki kuwa mshambuliaji aliyefiti kuongoza safu ya ushambuliaji ya Liverpool.

Huku wakiwa na alama 14 na kushika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi, Liverpool inatarajia kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuingia kati ya timu nne za juu (top four) kwenye msimamo wa ligi hiyo na kupunguza “gap” la alama 18 na vinara Chelsea.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anakibarua kizito cha kuiondoa Liverpool kwenye wimbi la kupoteza mechi kwani katika mechi nane za ligi zilizopita Liverpool ameshinda michezo miwili tu huku akitoka sare michezo miwili na kufungwa michezo minne.

Takwimu zinaonyesha Liverpool katika michezo tisa iliyopita ya ligi wamefungwa jumla ya magoli 18 huku wakizuia mara moja tu nyavu zao kutokutikiswa (clean sheet) na katika michezo 10 iliyopita dhidi ya Palace wameshinda michezo sita, kutoka sare michezo mitatu na kufungwa michezo mmoja.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno; Gerrard, Can, Henderson; Coutinho, Sterling; Balotelli

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!