Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 November 2014
Sunday, November 23, 2014

Real Madrid wajichimbia kileleni mwa La Liga.



Na Oscar Oscar Jr

Mabingwa wa bara la Ulaya, timu ya Real Madrid jana iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya Eibar kwa mabao 4-0 huku mchezaji bora Dunia kwa sasa, Christiano Ronaldo akifunga magoli mawili na kufikisha jumala ya mabao 20 ya La Liga msimu huu ndani ya mechi 12 zilizopigwa mpaka sasa.

Baada ya mwanzo mbaya, Real Madrid sasa wamefikisha ushindi wao wa 14 mfululizo kwenye michuano yote wanayoshiriki msimu huu. 

Miamba hao walianza kujipatia bao la kwanza kupitia kwa mfungaji bora wa kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil, James Rodriguez licha ya Ronaldo na Benzema kuonekana kana kwamba walikuwa wameotea.


Ronaldo kisha aliongeza la pili kwa kwa shuti kali lililomruka kipa wa Eibar Xabi Irureta  muda mfupi kabla ya mapumziko. Benzema alifunga la tatu dakika 20 kabla ya mechi kumalizika kabla ya Ronaldo tena, kukamilisha ushindi kwa kufunga kupitia mkwaju wa penalti. 

Ushindi huo umewarejesha Real kileleni mwa La Liga huku wakiwa na alama 30 na kufuatiwa kwa karibu na mahasimu wao timu ya Barcelona ambao wana alama 28 na nafasi ya tatu, anakamatwa na mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya Atletico Madrid ambao ushindi wao wa jana umewafanya wafikishe alama 26.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!