Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 November 2014
Saturday, November 29, 2014

Chelsea wakaribia udhamini mpya.


Na Chikoti Cico.

Timu ya Chelsea ambayo inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza, huku ikiwa haijafungwa mchezo wowote toka msimu wa 2014/15 kuanza inakaribia kupata udhamini mpya wa jezi toka kampuni ya Turkish Airlines.

Shirika hilo linalojihusisha na safari za ndege liko kwenye maongezi ya kuiadhamini timu hiyo kutoka London katika dili linalotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Chelsea ambayo kwasasa jezi zake zinadhaminiwa na kampuni ya simu ya Samsung, ambayo thamani ya udhamini wake ni paundi milioni 18 kwa mwaka inatarajiwa kuwa na udhamini wa kiasi cha paundi milioni 25 kwa mwaka kutoka Turkish Airlines.

Udhamini huo wa Turkish Airline utakuwa wa pili kwa ukubwa kwenye ligi kuu nchini Uingereza hivyo kuifanya timu ya Chelsea inayomilikiwa na Mrusi, Roman Abramovich kuwa juu ya Liverpool na Arsenal  katika udhamini wa jezi.

Pamoja na matarajio ya kukamilika kwa dili hilo la udhamini kutoka kwa Turkish Airlines, bado timu ya Chelsea itakuwa nyuma ya Manchester United kwa thamani ya udhamini wa jezi.

United ambao jezi zao zinadhaminiwa na kampuni ya magari ya Chevrolet, mkataba ulioanza msimu huu una thamani ya paundi milioni 53 kwa mwaka.
co

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!