Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Uchambuzi: Chelsea vs West Bromwich Albion




Na Chikoti Cico

Katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza mwisho wa juma hili timu ya Chelsea inatarajiwa kuumana na West Brom mchezo utakaopigwa jijini London kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote wa ligi kati ya michezo 11 waliyocheza wanatarajia kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kujichimbia kileleni bila kuharibu rekodi hiyo ya kutofungwa.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara kwasasa yuko fiti na anatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji ya Chelsea, mpaka sasa Costa ana magoli 10 katika mechi tisa alizoichezea Chelsea huku akishika nafasi ya pili kwenye listi ya wafungaji bora wa Uingereza.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajia kuondoa rekodi mbaya dhidi ya West Brom kwenye michezo ya ligi ya Uingereza kwani katika mechi tano zilizopita, Chelsea waliyokutana na West Brom wameshinda mchezo mmoja tu huku wakitoka sare michezo miwili na kufungwa michezo miwili.

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Ramires; Hazard, Oscar, Willian, Costa

West Bromwich Albion ambao wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 13 wanatarajia kuwakosa mabeki Jonas Olsson na Sebastien Pocognoli mabao ni majeruhi ila kurejea kwa kiungo Craig Gardner aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu kutaweza kuiongezea nguvu West Brom kwenye mchezo huo.

Kocha wa West Brom Alan Irvine ataingia kwenye mchezo kutafuta alama tatu muhimu huku akitafuta ushindi wake wa tatu ugenini lakini pia kujaribu kuondoa rekodi mbaya ya West Brom kwenye ligi ya Uingereza kwa kucheza michezo 14 iliyopita na kushinda michezo mitatu tu.

Kikosi cha kocha Alan Irvine kinaweza kuwa hivi: Foster; Wisdom, Dawson, Lescott, Davidson; Dorrans, Morrison, Gardner, Brunt; Sessegnon, Berahino

Takwimu zinaonyesha katika michezo 116 ya ligi kati ya Chelsea dhidi ya West Brom, Chelsea imeweza kushinda michezo 50, kutoka sare michezo 29 na West Brom kushinda michezo 37.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!