Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 November 2014
Friday, November 21, 2014

Mourinho asema Cech haendi kokote.


 Na Oscar Oscar Jr

Baada ya habari kuenea hivi karibuni kumuhusu golikipa wa Chelsea, Peter Cech kuhama klabu hiyo, Kocha Jose Mourinho amekanusha madai hayo na kusema kuwa hakuna ofa yoyote ambayo imefika ofisini kwake na hivyo anashangaa kuona blogs na Websites mbalimbali zikiandika juu ya kupita huyo kuondoka.

Peter Cech amekuwa akihusishwa kuhamia klabu za PSG, Real Madrid, Arsenal na Ac Millan. Mourinho amezungumza hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari kueleke mchezo wao wikendi hii dhidi ya klabu ya West Bromwich Albion unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 12:00 jioni kwenye dimba la Stanfford Bridge.

Cech ambaye alikuwa kipa namba moja wa klabu hiyo na kuwa sehemu ya mafanikio, amejikuta akipoteza nafasi ya kwanza kwenye kikosi cha Mourinho msimu huu kufuatia ujio wa Thibout Courtois ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Atletico Madrid kwa misimu kadhaa.

Cech ameanza mechi nne tu msimu huu kwenye mashindano yote ambayo Chelsea imeshiriki. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, amedaiwa kutofurahia kitendo cha kuwekwa benchi na anataka kuondoka ili kupata timu itakayo muhakikishia nafasi ya kucheza ambayo Chelsea ameipoteza.

Pamoja na kupoteza nafasi ya kwanza kwenye klabu yake, Cech ameendelea kuitwa kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa, Jamhuri ya Cech na ameanza kwenye mechi zote nne za kufuzu kwa michuano ya Euro 2016.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!