Sturridge pigo tena kwa Liverpool
Na Oscar Oscar Jr
Wakati wapenzi na mashabiki wa timu ya Liverpool wakianza kupata matumaini ya timu yao kumkaribisha mshambuliaji Daniel Sturridge, hali ya hewa imechafuka baada ya mshambuliaji huyo kuripotiwa kuumia tena wakati akiwa mazoezini.
Mchezaji huyo aliumia mara ya kwanza mwezi Septemba akiwa na timu ya taifa ya Uingereza kabla ya kuumia tena mwezi Octoba. Sturridge anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo ili kubaini ukubwa wa tatizo lililomtokea siku ya Jumanne na katika mechi 14 ambazo Liverpool imecheza bila mchezaji huyo, imeshinda mechi nne pekee.
Sturridge ambaye amewahi kucheza kwenye klabu za Manchester City na Chelsea, alijiunga na Liverpool wakati wa dirisha dogo msimu wa 2011/2012 huku akicheza msimu uliopita kwa kiwango cha juu mno na kufunga magoli 21 ya ligi kuu.
Hii sio habari nzuri kwa wanaLiverpool hasa ukizingatia kuwa, mshambuliaji Mario Balotelli ameumia pia akiwa na timu yake ya taifa ya Italia na kuna uwezekano ukakosa mchezo wao wa wikend hii watakapopambana na timu ya Crystal Palace.
Liverpoo kwa sasa inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kukusanya alama 14 katika michezo 11 ambayo wamecheza hadi sasa.
Mechi yao inayofuata itakuwa dhidi ya Crystal Palace ambao wako kwenye nafasi ya 18 huku wakiwa na alama tisa pekee.
0 comments:
Post a Comment