Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 November 2014
Thursday, November 20, 2014

Sababu za kuifanya Yanga kutwaa Ubingwa msimu huu.



 Na Samuel Samuel

Kombe la ligi kuu Tanzania bara linashikiliwa na timu ya Azam ambayo ilifanikiwa kufanya vema msimu uliopita kwa kujikusanyia alama 62 huku Yanga, wakiambulia nafasi ya pili baada ya kupata pointi 56 na Mbeya City wakikamata nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 49.

Yanga wanaonekana kutaka kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya 25 msimu huu ingawa mambo yanaonekana kuwa magumu kutokana na kuongezeka ushindani na pia, bado timu hiyo licha ya kukusanya pointi 13 na kushika nafasi ya pili, hawachezi vizuri.

Kuna mambo kadhaa ambayo Yanga wanapaswa kuyafanyia kazi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa. Kwanza kabisa, Kocha Maximo katika benchi lake la ufundi anahitaji kocha msaidizi ambaye ni mzawa anaelijua soka la Tanzania kwa marefu na mapana yake. 

Leonardo ana msaidia Maximo katika masuala ya kiufundi ila sizani kama ni msaada linapokuja suala la experience ya ligi, saikolojia ya wachezaji wazawa na utamaduni halisi wa soka la kitanzania. 

 Pili, Maximo anahitajika kupata namba sita mwenye uwezo mkubwa kuliko anavyocheza Mbuyu Twite sasa. Twite ana makosa mengi hasa katika kupandisha timu na kuziba makosa ya kiungo mchezeshaji pale anapozidiwa na majukumu. 

Kocha Jose Mourinho ameitengeneza Chelsea kusimama katika muhimimili wa namba sita, mashambulizi yanasukwa na sita na kukaba kunasimamiwa vyema na sita. 

Twite anatakiwa kurudi namba mbili. Kuendelea kumtumia Jaja kama mshambuliaji pekee pale kati ni kuzidi kuukataa ubingwa, Jaja ni mzuri endapo tu Maximo ataamua kushambulia kupitia pembeni na hapo inabidi awe na winga makini wenye kasi na uwezo wa kutoa pasi nzuri za mwisho. 

Mpeleke Ngasa kulia, Msuva kushoto halafu muamini Kiiza kama kiungo mshambuliaji. Kwa namna Yanga inavyocheza kwa sasa, wanahitaji mshambuliaji mzawa kupewa nafasi. Wachezaji kama Jerryson Tegete na Said Bahanuzi, wanaweza kucheza vema kwenye mfumo huo kuliko Jaja.

Mwisho, kocha Maximo kule mbele ili awe sawa anatakiwa kutengeneze kombinesheni ambayo itamruhusu Niyonzima kucheza soka lake lote ambalo Mungu kamjalia mguuni mwake na kichwani. 

Acheze na saikolojia ya Mnyarwanda huyu ili afurahie mpira kuliko ilivyo saa na kama hilo haliwezekani, ni bora kusajili kiungo mwingine na kumruhusu Niyonzima kuondoka kwenye klabu hiyo.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!