Na Chikoti Cico.
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney akaribia kufikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Sir Bobby Charlton ya magoli 49 hii ni baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Scotland ambao timu ya taifa ya Uingereza iliupata katika mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa kwenye uwanja wa Celtic Park nchini Scotland.
Rooney ambaye katika mechi iliyopita ya kufuzu kwa michuano ya EURO 2016 dhidi ya Slovenia alitimiza michezo 100 na kuwa kati ya wachezaji tisa walioichezea timu ya taifa ya Uingereza na kufikisha idadi ya michezo hiyo ameweza kufikisha magoli 46 katika michezo 101 aliyoichezea timu ya taifa ya Uingereza.
Rekodi ya mfungaji bora wa muda wote ya timu ya taifa ya Uingereza mpaka sasa inashikiliwa na Bobby Charlton aliyefunga magoli 49 akifuatiwa na Gary Lineker mwenye magoli 48 huku Rooney akishika nafasi ya tatu akiwa na magoli 46.
Huku mshambuliaji huyo wa Uingereza akikaribia kufikia rekodi hiyo ya Sir Booby Charlton pia anaikimbiza rekodi ya kipa wa zamani wa Uingereza Peter Shilton ya kuwa mchezaji aliyeichezea michezo mingi timu hiyo ya taifa inayofundishwa na kocha Roy Hugdson.
Mpaka sasa Rooney ameshacheza michezo 101 huku ikiwa bado michezo 24 kufikia rekodi ya michezo 125 ambayo Shilton aliichezea Uingereza kabla ya kustaafu.
0 comments:
Post a Comment