Arsenal wachezea kichapo mbele ya Man United
Na Oscar Oscar Jr
Hatimaye rekodi ya timu ya Arsenal kutopata ushindi mbele ya Manchester United kwa muda mrefu, imeendelea kuwaandama baaada ya hapo jana kujikuta wakichezea kichapo ch mabao 2-1 ndani ya dimba la Emirates.
Kikosi cha Manchester United kiliingia uwanjani kwa kutumia mfumo ule ule wa 3-4-3 huku Gunners, wakiendelea na moja kati ya mifumo ya ushambuliaji inayotamba duniani kwa sasa wa 4-3-3.
Arsenal pengine walitakiwa kuumaliza mchezo huo kwenye dakika 45 za awali baada ya kuutawala mchezo karibu kwenye kila idara huku lakini, ilishuhudia wachezaji wake wakipoteza nafasi nyingi za wazi.
Alex Chamberlain, Alex Sanchez na Welbeck kwa nyakati tofauti waliweza kupata nafasi za wazi kabisa za kufunga lakini hawakuweza kufanya hivyo huku golikipa wa Manchester United, David De Gea akiendelea kuwa shujaa wa mchezo.
Manchester United ambao walianza na Ukuta wa Chris Smalling, Blackett na MacNair walijikuta kwenye wakati mgmu baaada ya washambuliaji wa Arsenal kuliandama lango lao kwa presha kubwa lakini bado waliendelea kuwa na nidhamu nzuri ya mchezo kitu ambacho kilikuwa na faida kwao.
Mchezo ulishuhudia pia baadhi ya wachezaji wakishindwa kumaliza dakika zote 90 za mchezo huku kwa upande wa Manchester United, walimkosa beki wao Luke Shaw dakika za mwanzo kabisa wakati Arsenal, walimpoteza kiungo Jack Wilshere na kipa Szczesny.
Bao la kujifunga la Kieran Gibbs na bao kali kutoka kwa Wayne Rooney, yalitosha kuwezesha Manchester United kurejea katika nne bora Ligi kuu ya Uingereza kwa kuwacharaza Arsenal 2-1 Jumamosi.
Bao la Gibbs mnamo dakika ya 56 na lile la dakika ya 85 kutoka kwa Rooney, yalitosha kuwapatia United alama tatu muhimu. Arsenal msimu huu walikuwa hawajapoteza mchezo wowote nyumbani lakini Man United pia, walikuwa hawajashinda ugenini.
Nguvu mpya wa Arsenal, Olivier Giroud aliadhimisha kurejea kwake baada ya kuuguza jeraha kwa kufunga bao dakika ya 95, lakini United waliendelea kuwa imara katika kujilinda na kuwaacha vijana hao wa Wenger wakiwa alama 15 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo timu ya Chelsea huku wao wakiwa nambari nane kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kwa bahati mbaya, timu hiyo ya Arsene Wenger ilipoteza kiungo wa kati muhimu Jack Wilshere na kipa Wojciech Szczesny walioumia, zikiwa ni siku nne pekee kabla ya mechi muhimu ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinakamilika, United 2-1 Arsenal na sasa mshambuliaji na nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyeifunga Arsenal magoli mengi (11) katika historia ya ligi hiyo.
0 comments:
Post a Comment