Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 February 2017
Saturday, February 04, 2017

DRAXLER AMUITA MESUT OZIL LIGUE 1


Na FLORENCE GR

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani anaecheza katika klabu ya PSG Julian Draxler ameweka wazi matamanio yake ya kutaka kumuona mchezaji mwenzake wa Ujerumani Mesut Ozil anaekipiga katika timu ya Arsenal ya uingereza akitua katika miamba hiyo ya Ufaransa.

Draxler mwenye miaka 28 ameonyesha kiwango cha hali ya juu kwa miamba hao wa Parc de Princes tangu alipojiunga na mabingwa hao wa ufaransa akitokea klabu ya Wolfsburg ya nchini ujerumani katika kipindi cha usajili mwezi January na kufanikiwa kufunga magoli manne katika mechi sita za mashindano mbalimbali mpaka sasa.

Akiulizwa na television ya BeIN Sports  chini ufarasana kuwa ni mchzaji gani anaecheza nae timu ya taifa ya ujerumani angependa ajiunge na PSG Draxler alisema waziwazi kuwa angependa kumuona rafiki yake Mesut Ozil akisajiliwa na miamba hiyo.

Ozil amebakiza msimu mmoja tu kwenye  mkataba wake wa sasa  huku mazungumzo na kuongeza mkataba mwingine yamesimama kwa muda.

Akiongelea mustakabli wa maisha yake ndani ya Arsenal Ozil mwenye miaka 28 alisema kuwa anafuraha kusaini mkataba mwingine lakini klabu yake lazima itambue kuwa anahitaji kujua Mustakabali wa kocha Arsene Wenger ambae mkataba wake unaisha mwezi June mwaka huu.

Pia Draxler alipouliza kwanini ligi ya ufaransa imekuwa si sehemu maarufu kwa wachezaji wa Ujerumani kucheza soka ,alijibu kuwa ' hata mimi sijui kwanini wapo wachache hivi' aliendelea kusema kuwa 'Bundesliga imeendelea kuwavutia sana wachezaji wa kijerumani , nimechagua kuja hapa ili kuwa na uzoefu katika nchi nje ya ujerumani'.

Mchezaji huyo aliwashauri wachezaji wa kijerumani kwenda kucheza soka kunako ligi kuu ya ufaransa Ligue 1 bila kuwa na mashaka yoyote yale.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!