MOURINHO AIPIGA DONGO BAYERN MUNICH
Na FLORENCE GR
Kwa kile kinachoonekana kama kuipiga dongo ligi ya ujerumani kocha wa Manchester Uinted Jose Mourinho amsema kuwa ligi kuu ya nchini ungereza ni vigumu sana kununua mchezaji bora kutoka kwenye timu ambayo mnapigania ubingwa kama vile Bayern Munich inavyofanya kwa Borussia Dortmund.
Kwa miaka ya hivi karibuni Bayern Munich imekuwa na tabia ya kusajili wachezaji nyota wa wapinazni wao wakubwa Borussia Dortmund .
Lakini Mourinho amesema kuwa kuongezeka kwa ushindani katika ligi kuu Uingereza kwa miaka ya hivi karibuni kilichofanya aliekuwa kocha wa Manchester united Sir Alex Ferguson kununua wachezaji kutoka timu kubwa kirahisi na kuwapekea Old Trafford .
Akiongea na waandishi wa Habari kuelekea mechi yao dhidi ya Leicester city Mourinho anasema kuwa ' kwa ujerumani Bayern Munich anaanza kushinda ligi katika kipindi cha majira ya joto, kila mwaka wanaaenda Dortmund na kununua wachezaji wao bora '
'Siku moja wakaenda kumnunua Robert Rewandowski, mwaka unaofata wanaenda kumchukua Mario Gotze, mwaka mwingine wanaenda kwa Mats Hummels ,kwahiyo wanashinda ligi majira ya joto'.
Mourinho alisema kuwa ni vigumu sana kwenda Tottenham Hotspur na kunua wachezaji wao bora wawili au kwenda Arsenal au Chelsea kusajili wachezaji wao bora kitu ambacho hawezi na anapenda sana hali hiyo.
Mourinho alisema kuwa muda wa kushinda ubingwa kwa kushambulia wapinzani wako kwa kununua wachezaji wake nyota umekwisha.
Jose Mourinho alijiunga na Manchester united akitokea klabu ya Chelsea ambapo alifukuzwa baada ya timu hiyo kufanya vibaya sana na tangu ajiunga na Manchester united amekuwa na wakati mgumu sana kwenye ligi kwani wamekuwa hawapati matokeo mazuri sana hivyo kujikuta wakishika namba sita kwenye simamo wa ligi kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment