Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

Yaya Toure ameaga kwa ushindi.


Na Oscar Oscar Jr

Mabao mawili yaliyofungwa na kiungo wa kimataifa wa Uingereza, James Milner yalitosha kuwapa ushindi wa bao 2-1 Manchester City katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa kombe la FA walipopambana na timu ya Sheffield Wednesday kwenye dimba la Etihad.

Manchester City katika mchezo huo ilikuwa kama maajabu baada ya kushuhudia wakicheza kwa takribani dakika 60 bila kuwa na shuti hata moja lililolenga goli lakini baada ya kuingizwa kwa  David Silva na Samir Nasri, mambo yalibadilika na City wakashika usukani.

Mabingwa hao wa FA wa mwaka 2011 walijikuta wako nyuma kwenye dakika ya 14 tu ya mchezo baada ya Nuhiu kuipatia  Sheffield Wednesday bao la kuongoza. 

Timu hiyo ya daraja la kwanza msimu huu ilifungwa mabao 7-0 na Manchester City mwezi Septemba mwaka jana kwenye mchezo wa Capital One Cup lakini, kwenye mchezo huu walionekana kuimarika zaidi.

Mchezo huo pia ulimjumuisha kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure ambaye alikuwa anacheza kwa mara ya mwisho kabla ya kuelekea kule Guinea ya Ikweta kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika ambayo yataanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!