Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2017
Saturday, January 28, 2017

KIGOGO MWINGINE NJE AFCON







Na FLORENCE GR

Michuano ya kombe la maifa ya Afrika AFCON imeendelea kushika kasi nchini Gabon mara baada ya robo fainali mbili kuchezwa hapo jana .

katika robo fainali ya pili baina ya Senegal dhidi ya Cameroon iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini Afrika kutokana na historia iliyopo kati ya timu hizo pamoja na Mastaa mbalimbali wanaochezea timu hizo hasa katika kikosi cha Senegal.

Cameroon ambao ni mabingwa mara nne wa kobe hilo waliingia katika mechi hiyo kama 'under dog' huku kikosi cha Senegal kikiongozwa na mchezaji ghali wa Afrika anayekipiga katika kikosi cha Liverpool Saido Mane walionekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini mambo hayakuwa rahisi kihivyo.

Cameroon ambao timu yao inaundwa na vijana wengi na wachezaji wasiokuwa na majina makubwa sana kama wale wa Senegal walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu kuanzia sehemu ya ulinzi hadi 'foward line' huku goli kipa kijana mweye umri wa miaka 21 Fabrice Ondoa akiwa katika kiwango cha juu baada ya kupangua michomo kadhaa iliyoelekezwa golini kwake.

Senegal wanapaswa kujilaumu wenyewe kwani walitengeneza nafasi nyingi katika mchezo lakini walishindwa kuzitumia kutokana na ukosefu wa umakini wa washambuliaji wake huku nyingine zikizuiliwa vizuri kabisa na Ondoa amabye ndiye aliekuwa 'man of the match" katika mcheo huo.

Mchezo huo ulilazimika kwenda dakika 120 mara baada ya dakika 90 timu hizo kushindwa kufungana huku goli kipa wa senegal Abdoulaye Diallo akilazimika kupangua mchomo wa Jacques Zoua katika dakika za majeruhi hivyo kulazimika mchezo huo kwenda kwenye 'matuta' baada ya kushindwa kufungana tena ndani ya dakika 30 za nyongeza.

Katika penati hizo ilikuwa piga nikupige ambapo katika penati ya tano nyota wa  Senegal Saido Mane ilishuhudiwa mkwaju wake ukiokolewa kwa umaridadi mkubwa na Fabrice Ondoa huku Vincent Aboubakar  akipiga penati ya ushindi kwa upande wa Cameroon na kufaya matokeo kusomeka senegal penati 4-5 cameroon.

Sasa Senegal inaungana na vigogo wengine walioaga mashindano hayo kama Algeria na Ivory cost waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Endapo Senegal wangeshinda mchezo wangekuwa wamelipa kisasi cha miaka 15 iliyopita baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati 3-2 na Cameroon mara baada ya kushindwa kufungana ndani ya dakika 120 katika fainali ya AFCON nchini Mali 

Katika robo fainali ya kwanza iliyowakutanisha Bukina faso dhidi ya Tunisia ilishuhudiwa Burkinabe wakiendeleza ubabe dhidi ya waarabu hao baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Burkina faso walilazimika kusubiri hadi dakika ya 81 pale  Aristide Bance alipofungua kalamu ya magoli mara baada ya kupiga shuti la chini chini ikiwa ni dakika tano tu tangu aingie kutoka benchi.

Prejuce Nakoulma alihitimisha goli la pili kunako dakika ya 84 baada ya Bukina faso kufanya shambulizi la kushtukiza mara baada ya wachezaji  wote wa Tunisia kwenda kushambulia na mpira kuokolewa ndipo Nakoulma alipompiga chenga goli kipa wa Tunisia Aymen Mathlouthi umbali wa mita 40  kabla ya kufunga hivyo kuwahakikishia Burkina faso kuendelea kuwepo nchini Gabon hadi siku ya mwisho ya mashindano hayo.

Sasa burkina Faso watacheza na mshindi kati ya Morocco dhidi ya Misri siku ya Jumatano huku Cameroon akisubiri mshindi kati ya DR Congo dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi.



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!