Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 January 2015
Sunday, January 04, 2015

Walcott arudi kikosi cha kwanza kwa ushindi.


Na Oscar Oscar Jr

Arsenal wameanza vizuri utetezi wao wa Kombe la FA ambalo walilitwaa msimu uliopita kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Hull City ambao msimu uliopita walifungwa bao 3-2 kwenye mchezo wa fainali.

Arsenal ambao walitoka kuchezea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Southampton weekend iliyopita kwenye mchezo wa ligi kuu, leo hii wameweza kujipoza machungu kwa mabao mazuri kutoka kwa Per Mertesacker 20 na Alexies Sánchez 82′ ambayo yalitosha kuwapeleka Gunners kwenye mzunguko wa nne wa michuano hiyo.

Arsenal ambao walifanikiwa kulitwaa taji hilo mara mbili mfululizo msimu wa 2001/2002 na 2002/2003, walifanikiwa kutawala mchezo huo kwa asilimia 54 huku mashuti yao 17 yakionekana kuliandama lango la Hull City.

Katika mchezo huo kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza, Theo Walcott aliweza kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Gunners kwa mara ya kwanza tangu alipoumia kwenye mchezo wa kuwania kombe hilo tarehe 4 January mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!