Siri yetu ni Kroos, tatizo lipo kwa Bale na Isco
Na Markus Mpangala
KUNA rah asana kuitazama Real Madrid ikicheza soka kipindi hiki. Rafiki yangu Oscar Oscar Jr anasema Real Madrid haikamatika kwa kipindi hiki. Ni kweli Los Blancos haishikiki. Timu imecheza mechi 11 na kupachika mabao 42 unataka nini kingine.
Kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wanacheza wakijiamini sana. Wachezaji wanacheza kwa utulivu na kupanga idadi ya mabao. Mechi mbili dhidi ya Liverpool naona mmejionea kiwango na ufundi wa hali ya juu. Pamoja na kiwnago chote cha Real Madrid, kuna siri moja tu muhimu ndani ya kikosi hicho. Siri yetu ni kumsajili Toni Kroos.
Sijui ni kwanini Pep Guardiola aliamua kumruhusu kuondoka, labda kwakuwa alimtegemea Philip Lahm na baadaye Sebastian Rode. Lakini ukweli ni kwamba Kroos ni siri kubwa ya ushindi wa Real Madrid. Kroos anapiga pasi kali na zenye macho mno kuliko kiungo yeyote pale Santiago Bernabeu. Bahati nzuri anacheza pamoja na kiungo matata sana Luka Modric.
Ushirikiano wa vijana hawa ni mtamu, na ikufurahisha kila sekunde unapoitazama Real Madrid. Mbio za kuwani ubingwa wa Hispania umeshika kasi. Atletico Madrid, Barccelona, Valencia ndizo timu zenye kuonesha uchu wa ushindi. Wale vijana wa Basque yaani Atletico Bilbao na Real Sociedad waendelee kuimarika, lakini Real Madrid ni habari nyingine.
Wakati tunamsifu Toni Kroos kuna kitu kingine kimeibuka kwa vijana wetu wawili Gareth Bale na Isco. Carlo Ancelotti ana mtihani mzito kadiri siku zinavyokwenda. Kwenye kikosi chake anao wachezaji wawili muhimu kwa kila mechi. Garteh Bale ambaye ni mchezaji ghali zaidi duniani na Isco aka Disco ambaye ni kinda ghali zaidi kwa Real Madrid.
Ukiwa na Isco katika timu yako basi unashambulia kwa utulivu na unamiliki mpira kwa uhakika sana. Isco ni mbunifu na kiungo mwenye kubadili matokeo ya mchezo.
Isco anaweza kusaidia ulinzi na kuwafanya viungo wakabaji Toni Kroos na Luka Modric wapate msaidizi. Kwa namna yoyote Isco ni mchezaji anayehitajika sana kwa Los Blancos pale inapohitaji kumiliki mpira kwa muda mrefu na ubunifu wake usiotumia nguvu nyingi.
Bale ni mchezaji anayehitajika pale timu inapohitaji nguvu nyingi kuweza kuwashinda wapinzani wake. Kwa mfano mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich ilimhitaji sana Gareth Bale kuliko Isco.
Kama Madrid itacheza mashambulizi ya kushtukiza na yenye kasi zaidi, basi Gareth Bale ni mchezaji mwafaka. Lakini unapocheza dhidi ya timu inayopiga pasi nyingi kama Liverpool aua Barcelona, basi unamhitaji sana Isco.
Bale amepona na anarudi uwanjani. Hasara moja kubwa ya kuwa na Bale uwanjani ni kutomudu jukumu la kusaidia ulinzi. Hii ina maana James Rodriguez ndiye anatakiwa kusaidia ulinzi, wakati Bale akiwa na jukumu la kushambulia pekee. Ubora wa Isco anapokuwa na James, haulingani kabisa kama wakipangwa James na Bale. Kama wanapangwa James na Bale ina maana kwamba ‘network’ ua ilinzi baina ya wawili hawa itakuwa tatizo na kuwalazimu mabeki wa pembeni kubaki nyuma zaidi.
Ni rahisi wapinzani wa Madrid kuwadhibiti kama wanakuwa na James na Bale. Ukiangalia emchi za Real Sociedad na Atletico Madrid tnaliona hilo. Sasa mtihani mkubwa unakuja wakati wa kufanya uamuzi, kati ya kumuuza Isco au Bale. Kibiashara Gareth Bale ni mchezaji sahihi wa Florentino Perez. Kiufundi Isco ni mchezaji muhimu sana wa Ancelotti na benchi lake.
Ukicheza mchezo wa kasi, unamhitaji Bale. Ukichemza mchezo wa taratibu unamhitaji Isco. Mtihani huu si rahisi kuumaliza, tukumbuke pale benchi kuna mhitimu wa Castilla, Jesse Rodrguez. Jesse ana kasi kama Bale. Lakini Jesse hajapevuka la Bale wala hana ufundi wa Isco. Utaona ili kuepuka mtihani huu lazima mmoja akae benchi.
Hasa ni pale unapocheza kamari ya kumwanzisha Bale au Isco kisha mechi ikawa mbaya. Lakini kwa kikosi hiki hakuna sababu ya kumhofia mpinzani yeyote.
Hivi ungekuwa kocha wa Real Madrid ungemuuza nani; Isco na Bale. Halafu umesikia Christopher Kramer ananukia Real Madrid? Mara zote Real Madrid inanukia tu. Kila mchezaji anavuta harufu ya marashi mazuri ya Los Blancos wajanja wa ‘town’.
0 comments:
Post a Comment