Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 January 2015
Thursday, January 08, 2015

Uchambuzi: JKT Ruvu vs Stand United; Azam Complex



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga dhidi ya timu ngumu ya Coastal Union, vijana wa kocha Felex Minziro watawakaribisha Stand United kutoka mkoa wa Shinyanga kwenye dimba la Azam Complex Jumamosi hii kwenye mchezo wa mzunguko wa 10 wa ligi kuu Tanzania bara.

JKT Ruvu ambao wanakamata nafasi sita wakiwa na alama 13, watahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo ili kuwafikia Mtibwa Sugar ambao ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na alama 16.

Mtibwa Sugar ambao wamecheza mechi nane pekee, kwa sasa wako Zanzibar wakishiriki michuano ya Mapinduzi Cup ambako wametinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuwatoa Azam Fc kwa mikwaju ya penalty siku ya Ijumaa jioni.

Stand United wao wanakamata nafasi ya tisa wakiwa na alama 11 lakini watataka kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote ugenini. 

Stand United wanaonekana kuwa wazuri sana ugenini kwani tayari walipata ushindi ugenini dhidi ya Mgambo JKT kule Tanga kabla ya baadaye kutoka sare na timu za Simba, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Polis Morogoro.

JKT Ruvu ni timu inayoonekana kukamilika na hata ukitazama takwimu zao, wanaonekana kufunga mabao nane mpaka sasa huku wao pia wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara nane. 

Stand United katika mchezo huo watamkosa kiungo mshambuliaji Harouna Chanongo ambaye mchezo uliopita dhidi ya Polis Morogoro alipewa kadi nyekudu.

Vijana hao maarufu kama "Chama la wana" tayari wamepata ushindi mara mbili na endapo kama wataibuka na ushindi kwenye mchezo wao, watafikisha pointi 14 na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuepuka presha ya kushuka daraja.

Ukitazama ubora wa kikosi cha JKT Ruvu na matokeo yao msimu huu ni wazi kuwa watakuwa wanapewa nafasi kubwa sana ya kuibuka na Ushindi kwenye mchezo huo lakini Stand United imekuwa ni timu ambayo inacheza kwa nidhamu ya hali ya juu hasa wanapokuwa ugenini na matokeo ya sare kwao sio mabaya. 

Stand tayari wamefunga mabao sita pekee kwenye mechi tisa ambazo wamecheza msimu huu, huku wao wakiruhusu mabao 10. Bado safu yao ya ushambambuliaji inahitaji kufunga zaidi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuibuka na ushindi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!